1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya kijeshi yasababisha vifo vya raia Nigeria

13 Januari 2025

Mashambulizi ya anga ya jeshi la Nigeria yaliyowalenga makundi ya watu waliokuwa na silaha katika eneo la kaskazini-magharibi lililokumbwa na mizozo yamesababisha vifo vya watu kadhaa.

https://p.dw.com/p/4p7iT
Jeshi la Nigeria.
Jeshi la Nigeria likiwa katika doria.Picha: Sunday Alamba/AP Photo/picture alliance

Jeshi limesema watu hao waliouawa kimakosawalikuwa ni wafanyakazi waliovalia sare za walinzi wa usalama wa jamii. Sulaiman Bala Idris, msemaji wa gavana wa jimbo la Zamfara amesema jeshi la anga la Nigeria lilikuwa linawalenga waasi katika eneo la Zurmi na maeneo ya Maradun katika jimbo hilo. 

Soma pia:Nigeria kuwaadhibu wanajeshi waliohusika na mashambulizi ya droni

Hii ni mara ya tatu jeshi la Nigeria linawauwa raia kimakosa katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja wakati wa mashambulizi ya anga kuwalenga watu wenye msimamo mkali na makundi ya waasi.

Kampuni ya utafiti wa kiintelijensia SBM, yenye makao yake mjini Lagos imesema mashambulio haya ya anga yamesababisha vifo vya takriban raia 400 tangu mwaka 2017.


Jeshi la Nigeria limesema wanajeshi wake wawili wanakabiliwa na kesi kwenye mahakama ya kijeshi juu ya mashambulizi hayo yaliyowauwa watu.