Nchini Kenya, jamii imetakiwa kuhakikisha kuna ufahamu wa kutosha kuhusu mianya iliopo kwenye sheria kuhusu dhuluma za kijinsia ili kuwalinda wavulana na wanaume. Hii ni kufuatia tetesi kutoka kwa mashirika ya kijamii kuwa, kinyume na haki za mtoto wa kike zinavyotetewa, mtoto wa kiume amepuuzwa, na hata haki zake kutozingatiwa katika sheria nyingi, hivyo kumuacha bila mtetezi anapopitia dhuluma.