Mashirika ya UN yaweka msimamo juu ya hali ya Gaza
16 Novemba 2023Matangazo
Taarifa ya mashirika hayo yakiwemo lile la Afya Duniani - WHO, na la misaada ya kiutu - OCHA imesema hatua za aina hiyo zinaweza kusababisha madhara kwa raia, ikiwemo vifo vya idadi kubwa ya watu, chini ya mazingira ya sasa katika ukanda huo uliozingirwa.
Naye Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk ameonya kwamba ukosefu wa nishati unazuia usambazaji wa misaada na pande zote za mzozo huo haziwezi kuyaita mauaji ya raia kuwa ni ya bahati mbaya.
Turk ameangazia madai ya kuwepo ukiukaji mkubwa wa haki katika vita hivyo vya Israel na Hamas ambao amesema unahitaji uwajibikaji kamili.