1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhuru wa Ukraine kuwa msingi wa makubaliano ya amani

16 Juni 2024

Mataifa 80 kwa pamoja yameunga mkono uhuru wa Ukraine kuwa msingi wa makubaliano yoyote ya amani ya kumaliza vita vya Urusi vilivyodumu miaka miwili.

https://p.dw.com/p/4h6lZ
Bürgenstock, Uswisi
Mataifa 80 yatia saini hati ya uhuru wa Ukraine kuwa msingi wa makubaliano ya amaniPicha: Michael Buholzer/REUTERS

Lakini mataifa mengine muhimu yanayoendelea katika mkutano unaojadili amani ya Ukraine unaofanyika Uswisi hawakuunga mkono hoja hiyo.

Makubaliano hayo ya pamoja yaliukamilisha mkutano wa siku mbili uliofanyika katika eneo la mapumziko la Bürgenstock bila kuhudhuriwa na Urusi ambayo haikualikwa, lakini washiriki waliokuwepo walitarajia Urusi iwepo ili kushiriki kwaajili ya amani ya maeneo hayo mawili. 

Mkutano wa kimataifa wa amani Ukraine wafungua Uswisi

India, Saudi Arabia, Afrika Kusini na Umoja wa Falme za Kiarabu zilizoshiriki mkutano huo kupitia mawaziri wa mambo ya kigeni na hata wajumbe wa viwango vya chini ni miongoni mwa mataifa ambayo hayakutia saini hati ya mwisho katika mkutano huo iliyojumuisha masuala ya usalama wa nyuklia,  usalama wa chakula, na ubadilishanaji wa wafungwa. 

Brazil ambae ni nchi mtazamaji haikutia saini hati hiyo lakini Uturuki ambae ni mpatanishi kati ya Urusi na Ukraine ilitia saini hati hiyo.