1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa masikini bado yanayumba baada ya UVIKO 19

14 Machi 2024

Ripoti ya Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa imesema mataifa mengi hivi sasa yanarejea katika hali ya kawaida baada ya janga la UVIKO-19, ingawa mataifa masikini zaidi yanazidi kudidimia.

https://p.dw.com/p/4dVMY
Das Leben in ehemaligen Pandemie-Hotspots heute
Kirusi cha Corona Picha: DW

Mkuu wa mpango huo Achim Steiner amesema jana kwamba utafiti huu ni ishara ya wazi kwamba pengo hivi sasa linaongezeka baada ya miongo miwili kuliposhuhudiwa mataifa tajiri na masikini yakikaribiana kimaendeleo.

Kitisho cha UVIKO aina ya JN.1 kimeongezeka duniani

Faharasa ya Maendeleo ya Kibinadamu ya shirika hilo ya tangu 1990 imeonyesha maendeleo kwenye nusu ya mataifa masikini zaidi yameendelea kuwa chini ya viwango vilivyokuwepo hata kabla ya UVIKO.

Mataifa hayo yenye viwango vya chini zaidi kuanzia mwaka 2022 yalikuwa ni Sierra Leone, Burkina Faso, Yemen, Burundi, Mali, Chad, Niger, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini and Somalia.