1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Armenia na Azerbaijan zakubaliana kusitisha mapigano

10 Oktoba 2020

Mataifa ya Armenia na Azerbaijan yamekubaliana kusitisha mapigano katika eneo la Nagorno-Karabakh

https://p.dw.com/p/3jibp
Berg-Karabach Stepanakert | Kämpfe
Picha: AP/picture-alliance

Katika taarifa yao wanadiplomasia wa juu kabisa wamesema  hatua hiyo ina lengo la kubadilishana wafungwa na miili ya waliopoteza maisha huku ikiongeza kwa kueleza kwamba ufafanuzi zaidi utatolewa baadae. Tangazo hilo linatolewa baada ya masaa 10 ya mazungumzo ya kidiplomasia yaliofanyika nchini Urusi, ambayo yaliratibiwa na Waziri wa Mambo ya Nje ya Urusi, Sergey Lavrov.

Lavrov amesema hatua hiyo ya kusitishia mapigano itafungua njia ya mazungumzo ya kuusuruhisha mgogoro huo. Mapigano hayo ya sasa kati ya  Azerbaijani na Armenian, ambayo yalianza Septemba 27 na kusababisha vifo vya mamia ya watu yanahusisha mzozo mkubwa kabisa wa wa miongo kadhaa kuhusu Nagorno-Karabakh. Eneo hilo ambalo kiasili ni sehemu ya Azerbaijan lakini limekuwa katika udhibiti ya jamii ya wachache ya Warmenia, tangu kumalizika kwa mapigano ya kujitenga ya 1994.

Je jitihada za Urusi zitazaa matunda?

Moskau Gespräche zwischen Armenien und Aserbaidschan über Berg-Karabach | Außenminister
Mawaziri wa nje wa Urusi, Azerbaijan na ArmeniaPicha: Russian Foreign Ministry Press Office/Tass/imago images

Mazungumzo kati ya mawaziri wa mambio ya nje ya Armenia na Azerbaijan yalifanyika kufuatia mwaliko wa Rais Vladimir Putin wa Urusi, ambae ametoa miito kadhaa ya usitishwaji mapigano kwa Rais Aliyev wa Azerbaijan na Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinian. Armenia ilisema ikio tayari kwa kustisha mapigano, wakati awali Azerbaijan ilitoa masharti ya kutekeleza jambo hilo kwa masharti ya Armenia kuyaondoa majeshi yake katika eneo la Nagorno-Karabakh, kwa kusisita kwamba kushindwa kwa jumuiya ya kimataifa kusuluhusha mzozo huo kidiplomasia kutaacha fursa moja ta kwa upande wao, ambayo ni matumizi ya nguvu.

Soma zaidi:Ufaransa itafanikiwa kuleta amani eneo la Nagorno-Karabakh?

Urusi iinafadhili mazungumzo ya amani kuhusu Nagorno-Karabakh sambamba na Marekani na Ufaransa kama wenyeviti wenza katika kile kinachoitwa kundi la Minsk, ambalo linafanya kazi chini ya udhamini wa Shirika la Usalama na Ushirikiano la Ulaya.