EU yafikia makubaliano kuhusu mageuzi ya sheria za uhamiaji
20 Desemba 2023Tangazo la makubaliano hayo limetolewa na Uhispania iliyoongoza majadiliano marefu ya kufikiwa mkataba utaokapunguza wimbi la wahamiaji, linalotajwa na wanasiasa wa Ulaya kuwa moja ya changamoto kubwa zinazoikabili kanda hiyo.
Mageuzi yaliyoridhiwa ni pamoja na kuharakisha mchakato wa kushughulikia maombi, kuanzisha vituo vya kuwazuia wahamiaji mipakani na kuwarejesha makwao wale ambao maombi yao yamekataliwa.
Soma pia: Ulaya njia panda kuheshi haki za binadamu au mipaka yake?
Makubaliano hayo pia yanaweka utaratibu wa kuyapunguzia mzigo mataifa ya kusini mwa Ulaya hususani Italia, Uhispania, Ugiriki na visiwa vya Malta ambayo yamekuwa lango kwa maelfu ya wahamiaji wanaojaribu kuingia Ulaya. Hata hivyo, mkataba huo utasubiri kuridhiwa na nchi zote 27 wanachama na bunge la umoja huo kabla ya kuanza kufanya kazi.