SiasaMarekani ya Kusini
Mataifa ya ulaya yaitaka Venezuela kuweka wazi matokeo
4 Agosti 2024Matangazo
Katika taarifa yao ya pamoja iliyotolewa jana Jumamosi, Ujerumani, Ufaransa, Italia, Poland, Uholanzi, Uhispania, na Ureno wameonesha wasiwasi wao mkubwa kuhusu hali ya Venezuela baada ya uchaguzi huo wa rais.
Kufuatia mashaka hayo nchi hizo zimetowa wito kwa serikali ya Venezuela kuyaweka hadharaini haraka matokeo yote ya kura ili kuakisi uwazi na uadilifu katika mchakato wa uchaguzi.
Baada ya uchaguzi wa Julai 28, mamlaka ya uchaguzi ya Venezuela ilimtangaza Rais Nicolás Maduro, ambaye amekuwa madarakani tangu 2013, kuwa mshindi. Hata hivyo, mpaka sasa haijachapisha matokeo binafsi ya kila wilaya zilizoshiriki mchakato huo.