1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa yakutana kujadili matumizi ya nishati ya nyuklia

21 Machi 2024

Viongozi wa ulimwengu wamekutana mjini Brussels katika mkutano wa kilele kuhusu nishati ya Nyuklia.

https://p.dw.com/p/4dz27
Ubelgiji, Brussels | Mkutano kuhusu nishati ya nyuklia
Viongozi wanaohudhuria mkutano wa nyuklia mjini Brussels Picha: Yves Herman/REUTERS

Unalenga kujadili masuala ya Nishati ya Nyuklia, kuangazia jukumu la nishati ya nyuklia katika kushughulikia changamoto za kimataifa za kupunguza matumizi ya nishati ya kisukuku, kuimarisha upatikanaji wa nishati, na kukuza maendeleo ya kiuchumi.

Mkutano huu ni wa ngazi ya juu zaidi kufikiasasa ukijikita kikamilifu kuangazia suala la nishati ya nyuklia.

Waziri Mkuu wa Ubelgiji Alexander De Croo anayeongoza mkutano huo pamoja na Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki, IAEA Rafael Mariano Grossi, amewaambia viongozi hao kwamba hawatakiwi kupoteza tena muda kuhusu mabadiliko ya tabianchi.

"Hatuwezi kupoteza muda linapokuja suala la kupambana na ongezeko la joto duniani. Changamoto tunayokabiliana nayo ni kubwa sana. Watoto wanahitaji kiasi kikubwa, salama na cha kutegemewa cha nishati isiyo na kaboni. Itatulazimu kuwahusisha wananchi na viwanda vyetu," amesema De Croo

Zaidi ya mataifa 30 kutoka Ulaya, Marekani, Brazil na China yameshiriki mkutano mkutano huo wa siku moja ulioandaliwa na IAEA kuhamasisha nyuklia kama chanzo cha nishati safi na ya kutumainiwa.