1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Asili na mazingiraKorea Kusini

Wanadiplomasia waonya kukosekana mkataba wa taka za plastiki

30 Novemba 2024

Wanadiplomasia wameonya Jumamosi hii kwamba mataifa mengi yanaweza yakasusia mazungumzo ya kimataifa yanayohusiana na uchafuzi utokanao na taka za plastiki.

https://p.dw.com/p/4nbcz
Taka ya plastiki
Plastiki kama hii zimekuwa tishio kubwa kwa usalama wa si tu binaadamu,bali pia wanyama Picha: Anette Jäger/imageBROKER/IMAGO

Wanadiplomasia wametoa onyo hilo wakati wajumbe wachache wanaendelea kupinga miito ya kujitolea kukabiliana na hali hiyo.

Karibu mataifa 200 yako Busan nchini Korea Kusini kwa majadiliano ya kuzuia uchafuzi huo, lakini juhudi zimekwama kutokana na kutokukubaliana na hasa katika kupunguza uzalishaji na kuondoa kemikali zinazoaminika kuathiri afya ya binaadamu.

Mataifa 100 yanaunga mkono hatua hiyo, lakini mengine hayaungi mkono hatua inayoelezwa kwamba itakwamisha kupatikana kwa suluhu dhidi ya uchafuzi huo.