Mataifa yataka kurefushwa usitishwaji mapigano Gaza
27 Novemba 2023Shinikizo za kimataifa zimeongezeka za kulitaka kundi la Hamas na Israel kurefusha muda wa makubaliano ya kusitisha vita Ukanda wa Gaza, wakati leo ikiwa ni siku ya mwisho ya kumalizika makubaliano hayo, yaliyofunguwa njia ya kuachiwa huru kwa wafungwa na mateka.
Rais wa Marekani Joe Biden amesemausitishaji vita unapaswa kuendeleakuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Gaza na kuachiliwa huru mateka zaidi wa Israel wanaoshikiliwa na wanamgambo wa Hamas.
Maafisa waaandamizi wa Umoja wa Ulaya na kutoka Jumuiya ya kujihami ya NATO pia wamepaza sauti zao kutowa mwito kama huo.
Makubaliano ya usitishaji vita yanatarajiwa kumalizika asubuhi ya kesho Jumanne, hali ambayo inatishia kuanza upya kwa mapambano makali baada ya siku nne za utulivu.
Chanzo kimoja kilichozungumza na shirika la habari la AFP kimesema, kundi la Hamas tayari limeonesha kuwa tayari kuendelea kusitisha vita kwa siku mbili hadi nne zaidi.