Waendesha mashtaka wa Ujerumani wamewafungulia mashtaka watu watatu kwa njama ya ujasusi. Mshukiwa mkuu, Dieter S., inaaminika kuwa ni mwanamgambo mkongwe wa kundi la wapiganaji wanaoiunga mkono Urusi nchini Ukraine, ambalo Ujerumani inalizingatia kuwa la kigaidi.