1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matatizo ya kiafya yachangiwa na kutokula mbogamboga

Oumilkher Hamidou7 Desemba 2010

Inasemekana Waafrika hawali matunda na mboga za majani vya kutosha. tatizo kubwa barani Afrika ni vitambi na unene, ugonjwa wa kisukari na magonjwa ya moyo na inasemekana yanahusiana na lishe duni.

https://p.dw.com/p/QSCh
Mbogamboga ambazo zinasaidia kujenga kinga ya mwili dhidi ya maradhi
Mbogamboga ambazo zinasaidia kujenga kinga ya mwili dhidi ya maradhiPicha: Fotolia/Olga Lyubkin

Jacky Ganry wa kituo cha utafiti wa kilimo nchini Ufaransa CIRAD katika kongamano Mjini Dakar ameseba nchi nyingi za Afrika, nusu ya watu wake wanauzito wa juu ama usio lingana na inavyotakiwa.

Na kusema Barani Afrika hali ni mbaya wastani wa upatikanaji wa matunda na mboga za majani si sawa na hali halisi ya kiwango kinachohitajika, Na kusema Shirika la Afya Duniani, WHO, limeweka wastani wa kiwango cha gramu 400 kwa siku.

Watu wengi wanaoishi mijini, maisha yanabadilika na mpangilio wa mlo pia unabadalika, ukingalinganisha na kutofanya mazoezi na upungufu wa kula matunda na mboga za majani, kunachangia kwa kiwango kikubwa kuongezeka kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile Kansa, shinikizo la damu, kisukari na magonjwa yote yanayohusiana na moyo.

Maeneo ya mijini watu wengi ni wanene ukilinganisha na vijijini ambako si sana.

Barani Afrika katika nchi ya Ethiopia kulikuwa na idadi ndogo ya watu wanene lakini asilimia 31 ya vifo vyote nchini humo kwa mwaka 2005 yalitokana na magonjwa yasiyo yakuambikiza

Nchini Senegal mnamo mwaka 1980 kulikuwa na kesi 200 tu za ugonjwa wa kisukari kwa mwaka, lakini ugonjwa huo umeongezeka kufikia wagonjwa 2000.

Mtafiti huyo anasema kuongezeka kwa upatikanaji na matumizi ya matunda pamoja na mboga za majani Barani Afrika ni changamoto kubwa, kwa sababu ya kuongezeka kwa miji mikubwa, mabadiliko ya milo, kuongezeka kwa gharama ya vyakula na ubora wa wake.

Kongamano hilo liliandaliwa na shirika la chakula na kilimo kwa jili ya kutafuta ni jinsi gani wanaweza kusambaza mbongamboga na matunda kwa watu wengi na kwenye miji inayokuwa kwa haraka

Mkulima wa mbogamboga Chris Ojiewo kutoka kituo cha mbogamboga Duniani kilichoko nchini Tanzania amesema utapiamlo na unene barani afrika umekuwa mzigo mara dufu.

Amewataka waafrika kutumia mboga za majani za asili ambazo zinalimwa kwa urahisi na zina kiwango kikubwa cha virutubisho kuliko vyakula vingine ili kuweza kutatua tatizo la utapiamlo na unene.

Waafrika wengi wa tabaka la kati ambao ni wanywaji pombe na nyama choma. kuwashawishi waachane na vyakula hivyo na wale vyakula vya asili kama nyanya chungu ama nyanya mshumaa, ni kibarua kigumu sana.

Baadhi ya mboga za asili ni chungu, na hazimpi mtu hamu ya kula, lakini zinavirutubisho.

Wataalamu wa virutubisho wanafanya kazi kubwa ya kuwafundisha wanawake jinsi ya kupika mbogamboga na kutayarisha matunda, lakini mara nyingi inamaanika ni kwa ajili ya kuwa na umbo jembamba kutokana na kiwango cha virutubisho kilichono.

Ojiewo anasema mtu mmoja anatakiwa kula gramu 16,300 za kabechi kwa mahitaji ya siku nzima kwaa jili ya Vitamini A, lakini hili linaweza fanikiwa kwa gramu 300 tu za Nyanya chungu.

Ushawishi wa mboga za majani umefanikiwa sana katika nchi za Afrika Mashariki ambapo maduka makubwa yanayouza vyakula taratibu yanapunguza mtindo wa kuuza bidhaa za mboga mboga zinazoagizwa kutoka nje na badala yake kuuza zile zinazolimwa ndani nchini.-

Mwandishi: Fatma Matulanga/AFPE

Mhariri: Abdul-Rahman