1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matayarisho ya michuano ya AFCON yakamilika

16 Januari 2015

Fainali za kombe la mataifa ya Afrika , AFCON, zinaanza rasmi (kesho)17.01.2015, ambapo timu 16 zilizofuzu zitawania taji hilo la juu kabisa barani Afrika.

https://p.dw.com/p/1ELXY
Äquatorialguinea Bata Stadion
Uwanja wa mjini Bata ambao umekamilikaPicha: picture-alliance/dpa/abaca

Magari ya kuchanganya saruji, malori makubwa makubwa , matrekta, na kelele kubwa za ujenzi zilikuwa ni sauti za kawaida kabisa katika muda wa miezi miwili iliyopita nchini Guinea ya Ikweta katika matayarisho ya fainali hizo.

Tangu pale nchi hiyo ndogo ya Afrika magharibi kuchukua jukumu la kuandaa mashindano hayo ya kila baada ya miaka miwili barani Afrika kutoka Morocco ambayo ilijitoa kuandaa mashindano hayo kutokana na hofu ya kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola, mbinyo ulikuwa mkubwa kuweza kukamilisha maandalizi hayo katika kipindi kifupi. Hususan katika viwanja.

Äquatorialguinea Fußball Nationalmannschaft
Timu ya taifa ya Guinea ya Ikweta wenyeji wa mashindano ya AFCON 2015Picha: picture-alliance/dpa/Stringer

"Kuhusiana na masuala ya umeme, tumekamilisha kila kitu na tayari kwa matumizi, nguzo zote zimebadilishwa. Kazi imekamilika kwa asilimia 100."

Mhandisi Federico Songa anawajibika na ukarabati wa uwanja mkubwa wa kandanda katika mji mkuu Malabo, ambao pamoja na uwanja wa mjini Bata ambao miaka miwili nyuma ulikuwa ni uwanja wa mapambano wa kombe la mataifa ya Afrika, wakati Guinea ya Ikweta na nchi jirani ya Gabon zilishiriki kuwa wenyeji wa fainali hizo.

Matayarisho yamekamilika

Kazi ya matayarisho imekamilika , na viwanja viko tayari kwa mashabiki kuburudika na kandanda , amesema hivyo waziri wa nchi anayehusika na vijana na michezo Ruslan Obiang.

"Kazi zimekamilika uwanja wa Malabo na Bata. Lakini kuna miji mingine miwili , Mongomo na Ebebey, ambayo viwanja vyake vina uwezo wa kuingiza watazamaji 15,000."

LOG CAF 2012 Orange Africa Cup of Nations
Nembo ya shirikisho la soka barani Afrika CAF

Ni viwanja vidogo kwa mashindano ya kimataifa na vinahitaji marekebisho makubwa kama viwanja vingine viwili vikubwa. Uwanja mzima ni lazima kufanyiwa marekebisho , maeneo ya watazamani ni lazima kurekebishwa. Majani ya kiwanja yanaletwa kutoka Ulaya. Na hii ilichukua muda wa miezi miwili, anasema mwandishi wa habari za michezo Yves Oyono kutoka Gabon.

Si suala rahisi. Hali hii haijawahi kutokea kokote kule duniani. Pamoja na hayo viwanja havijakuwa changamoto kubwa anasema hivyo balozi Mari Druz Evuna Andeme.

"Kuhusiana na miundo mbinu, ilikuwa na maana ya ujenzi wa barabara kwenda katika viwanja hivi vidogo, ilikuwa si tatizo kubwa. Lakini tatizo ni nafasi ya kuwapatia malazi watu wengi kwa wakati huu."

Afrika Cup Fan von Äquatorialguinea
Shabiki wa timu ya taifa ya Guinea ya Ikweta , mwaka 2012.Picha: DW/N.K.Tadegnon

Mashabiki na viongozi wa timu

Mjini Mongomo kwa mfano kuna hoteli moja tu yenye vitanda 56. Hii haitoshi kwa timu za mpira , wasaidizi wao, viongozi, waandishi , pamoja na mashabiki wanaosafiri kuzishangiria timu zao. Maafisa wa miji hiyo wamejenga kwa muda mfupi nyumba maalum kwa ajili ya mashindano hayo ambazo zitagawiwa na mamlaka ya miji kwa watu watakaohitaji.

Miundo mbinu katika miji hiyo imekamilika. Pamoja na hayo nchi hiyo ilikuwa mwenyeji mwaka 2012 , kwa hiyo ina uzoefu na ujuzi, kuhusu utayarishaji wa mashindano kama hayo.

Mwandishi: Linda Staude / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri: Josephat Charo.