Mateka watatu walioachiliwa na Hamas wana afya njema
20 Januari 2025Emily Damari, Romi Gonen na Doron Steinbrecher ambao walitekwa wakati wa shambulio la oktoba saba mwaka 2023 waliachiliwa hapo jana Jumapili baada ya kushikiliwa na Hamas kwa zaidi ya miezi 15 katika Ukanda wa Gaza.
Israel kwa upande wake imewaachilia wafungwa 90 wa Kipalestina leo Jumatatu. Msemaji wa Hamas amethibitisha kuwa mateka wanne wa Israel wataachiliwa siku ya Jumamosi ijayo kama sehemu ya makubaliano ya kubadilishana mateka 33 kwa wafungwa 1,904 wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za Israel katika kipindi hicho ya wiki sita.
Katika hatua nyingine wapalestina wameanza kurejea katika makazi yao huko Gaza baada ya kusitishwa kwa mapigano ingawa wengi wanaeleza kwamba makazi yao yameharibiwa vibaya. Huyu ni Ahmed Al Akhrasa akisimulia jinsi alivyoyakuta makazi yake.
Hatua hiyo inajiri siku chache baada ya kufikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosimamiwa na wapatanishi ambao ni Marekani, Qatar na Misri.