1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matumaini ya EU baada ya uchaguzi wa Poland

Angela Mdungu
16 Oktoba 2023

Umoja wa Uaya unasema mabadiliko ya serikali nchini Poland yatakuwa ushindi kwa demokrasia huria. Ni baada ya upinzani nchini Poland kusherekea matokeo ya awali leo, yanayoonyesha umepata wabunge wengi.

https://p.dw.com/p/4Xb0Y
Kiongozi wa upinzani  nchini Poland Donald Tusk
Kiongozi wa upinzani nchini Poland Donald TuskPicha: REUTERS

Brussels inatumaini kuwa serikali mpya ya Warsaw itarahisisha kurejea kwa utawala wa sheria nchini humo.

Kamishna wa maadili na uwazi wa Umoja wa Ulaya Vera Jourova bado hajazungumza lolote kuhusu ushindi katika matokeo ya awali uliopata upinzani katika uchaguzi mkuu.

Kwa miaka mingi, Jourova amekuwa akikwaruzana na serikali ya Chama cha kihafidhina cha sheria na haki cha PiS kuhusu utawala wa sheria ulio hatarini nchini Poland.

Chama hicho kinachotawala kinachoongozwa na Jaroslaw Kaczynski kilikataa kubadilisha mageuzi ambayo mahakama ya Umoja wa Ulaya iliyataja kuwa ni kinyume cha sheria na kusababisha msururu wa kesi kutoka kwa ya Umoja huo.

Soma zaidi: Uchaguzi Poland: Morawiecki na Tusk wadai kushinda

Matokeo yake, Umoja wa Ulaya uliisimamisha Poland kutumia fedha za bajeti ya pamoja na ilipigwa faini kwa kushindwa kuheshimu hukumu ya mahakama ya haki ya Luxemburg.

Nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Ulaya zilianza pia kufungua kesi dhidi ya Poland, lakini hazikufika mbali. Wakati huo huo, sauti dhidi ya Umoja wa Ulaya na Ujerumani zilianza kusikika kutoka Poland. Hali hii inatarajiwa kukoma baada ya mabadiliko ya serikali ambayo huenda yakahusisha muungano wa vyama vitatu kuunda serikali ambavyo ni pamoja na Chama cha  Krikristo cha demokrasia, Chama cha Kiliberali na Chama cha Kijani.

Wapiga kura wakishiriki uchaguzi Poland
Wapiga kura wakishiriki uchaguzi PolandPicha: Onkar Singh Janoti/DW

Pyotr Buras, msomi kutoka Baraza la Ulaya la sera za kigeni  anatarajia serikali chini ya mkuu wa chama cha Civic Platform  Donald Tusk kuwa na jukumu muhimu la kuimarisha mahusiano na washirika muhimu katika Umoja wa Ulaya.

Buras ameiambia DW kuwa, pasi na shaka, serikali mpya itahitaji wiki kadhaa kujiweka sawa madarakani na kisha kujaribu kuwaondoa watendaji waaminifu wa chama cha PiS katika nafasi nyeti za utawala, vyombo vya habari, mahakama  na makampuni yanayomilikiwa na serikali.

Mwenyekiti mwenza wa kundi la chama cha kijani katika Bunge la Ulaya ambaye amekuwa akifuatilia yanayoendelea Poland, Terry Reintke,  amesema mivutano kati ya Poland na Ukraine ambazo zimekuwa zikizozana kuhusu usafirishaji wa nafaka kutoka na kupitia Poland nayo itapungua. Anasema anatarajia kuwa nchi hiyo itakuwa mshirika wa kutegemewa wa Umoja wa Ulaya inayoliunga mkono taifa Jirani la Ukraine iliyo kwenye mgogoro na Urusi.