Mauaji ya Bhutto kuzusha tofauti za kikabila Pakistan
6 Januari 2008Mauaji ya Benazir Bhutto, kiongozi mwenye ushawishi mkubwa wa chama cha Pakistan Peoples Party, PPP, na aliyekuwa mara mbili waziri mkuu wa Pakistan, yameisukuma nchi hiyo katika hatari ya kutumbukia katika mgawanyiko wa kikanda na kikabilia.
Benazir Bhutto alijulikana kama kiongozi aliyungwa mono na idadi kubwa ya watu katika majimbo yote manne ya Pakistan, yakiwemo Punjab, Balochistan, North West Frontier na jimbo alikotea la Sindh.
Mkoa wa Punjab, ambao ni mkubwa kiidadi na kiraslimali, umekuwa kwa muda mrefu ukiliaumiwa kwa kuingilia haki za majimbo mengine. Ushawishi mkubwa wa jimbo hilo dhidi ya majimbo mengine pia unasababishwa na ukweli kwamba viongozi wa ngazi za juu katika jeshi la Pakistan kitamaduni huteuliwa kutoka mkoa wa Punjab.
Mumewe marehemu Benazir Bhutto, Asif Ali Zardari, na viongozi wengine wa mkoa wa Sindh wamekabiliwa na kibarua kigumu cha kuondoa vitishi dhidi ya chama cha PPP, wakihubiri umojha wakati kukiwa na hali ya wasiwasi nchini Pakistan iliyosababishwa na mauaji ya Benazir Bhutto mnamo tarehe 27 mwezi Disemba mwaka jana, ambapo kabila moja liliinuka dhidi ya kabila lengine.
Katika mazishi ya Benazir Bhutto, waombolezaji walibeba bango lilolukuwa na maneo yaliyosema ´Pakistan nakhabey´yaani hatuitaki Pakistan, hivyo kumpa kazi ngumu Zardari kusisitiza kwenye mikutano mingine na mikutano na waandishi wa habari kwamba chama cha PPP kinataka nchi moja iliyoungana na hakipingani na ushawishi wa jeshi.
Akizungumza juu ya maandamano ya nchi nzima na machafuko ya kikabilia, rais wa Pakistan Pervez Musharraf katika hotuba yake kwa taifa mnamo tarehe 2 mwezi huu alisema vikosi vya wanajeshi viko tayari katika mkoa wa Sindh kukabiliana vilivyo na wavunjaji wa sheria na wachochezi. Hotuba kali ya rais Musharraf iliwakasirisha wengi. Kiongozi wa chama cha PPP mkoani Punjab, Shah Mehmood Qureshi, alisema hotuba ya rais Musharraf ilishusha hadhi ya Pakistan akisema hakukuwa na haja ya kutumia maneno makali bila kutofautisha kati ya wahalifu na waombolezaji.
Qadir Magasi, kiongozi wa kitaifa mkoani Sindh ambaye ni mwenyekiti wa chama cha mkoani humo cha Taraqqi Passand, STPP, amelimbia shirika la habari la IPS kwamba Benazir Bhutto aliuwawa kwa sababu alikuwa akitokea mkoa wa Sindh na pia hakuwa tayari kulinga mkono jeshi la Pakistan. Kosa la Bhutto ni kwamba alizungumzia kuhusu demokrasia, mamlaka ya bunge na katiba.
Magsi ambaye pia ni kiongozi mwenye ushawishi mkubwa katika vuguvugu la muungano wa vyama, All Parties Democratic Movement, APDM, na pia katika chama cha Pakistan Opressed Nation´s Movement, kinachodai mikoa yote iwe na usawa, anaamini hatua ya Benazir Bhutto kuwapendelea wakaazi wa jimbo la Balochistan na ukosoaji mkali wa mauaji ya Nawab Akbar Bugti kwenye uvamizi wa kijeshi katika mkoa wa Sindh, yamewakasirisha viongozi wa serikali ambao wengi wao wanatokea jimbo la Punjab.
Lakini ukweli kwamba Benazir Bhutto aliuwawa mjini Rawalpindi mkoani Punjab, ambao unadhibitiwa na jeshi, umezusha hofu kwamba Pakistan huenda ikapasuka katika misingi ya kikabila. Hofu za aina hiyo hazipaswi kupuuzwa kwani mnamo mwaka wa 1971 tofauti za kikabilia zilizusha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha Paksitan kupoteza jimbo lake la mashariki ambalo hivi leo ni Bangladesh.
Imegunduliwa kwamba viongozi wa ngazi za juu wasiotokea jimbo la Punjab hatimaye huuwawa mjini Rawalpindi kwa kasi fulani. Mawaziri wakuu wawili wa zamani, babake Benazir, Zulfikar Ali Bhutto na Liaquat Ali Khan, pia waliuwawa mjini Rawalpindi.
Muasisi na kiongozi wa chama cha Muttahida Quami Movement, MQM, Altaf Hussain, ambaye hivi sasa anaishi uhamishoni nchini Uingereza, alitoa taarifa muda mfupi baada ya Bhutto kuuwawa. ´Ningependa iingie katika vitabu vya kumbukumbu kwamba mauaji haya ni ya tatu ya waziri mkuu anayetokea mkoa wa Sindh,´ alisema Hussain. Aidha kiongozi huyo alisema mauaji ya Bhutto ni kitendo cha kuiharibu nchi na kujenga hisia za kutengwa miongoni mwa wakaazi wa mkoa wa Sindh.