1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoAustralia

Mauzo ya tiketi za Kombe la Dunia yamefikia milioni 1.6

1 Agosti 2023

Shirikisho la Kandanda Duniani - FIFA limesema kuwa mauzo ya tiketi za Kombe la Dunia la Wanawake yamefikia milioni 1.6 katika mechi 38 za kwanza za kinyang'anyiro hicho nchini Australia na New Zealand.

https://p.dw.com/p/4UceA
Wachezaji wa Australia wakishangilia bao la pili la Hayley Rasos 16 la Australia wakati wa mechi ya Kundi B ya Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake la 2023 Uwanja wa Mstatili wa Melbourne AAMI Park mjini Melbourne, Australia.
Wachezaji wa Australia wakishangilia bao la pili la Hayley Rasos 16 la Australia wakati wa mechi ya Kundi B ya Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake la 2023 Picha: Noe Llamas/Sports Press Photo/IMAGO

FIFA imesema katika taarifa leo kuwa jumla ya mashabiki waliohudhuria mechi hizo wamefikia 982,975 na idaid hiyo itavuka milioni 1 kwa watazamaji kwenye mechi ya mwisho leo Jumanne ya Kundi E kati ya Marekani na Ureno kwenye uwanja wa Eden Park wenye uwezo wa kuchukua watu 50,000 huko Auckland, New Zealand.

Kinyang'anyiro hicho tayari kimevunja rekodi za wahudhuriaji kwa Kombe la Dunia la Wanawake. Mashindano ya mwaka huu yametanuliwa hadi timu 32 na yanajumuisha mechi 64.

Katika mechi nyingine za leo, za kukamilisha hatua ya makundi, Vietnam itacheza dhidi ya Uholanzi katika Kundi E wakati katika Kundi D China itaangusha na England nayo Haiti itaikaribisha Denmark