Mawakili watatu wa Navalny watiwa hatiani nchini Urusi
17 Januari 2025Matangazo
Mahakama nchini Urusi imewahukumu kifungo cha miaka mitatu hadi mitano mawakili wa aliyekuwa kiongozi wa upinzani nchini humo Alexei Navalny waliokutwa na hatia ya kujihusisha na kundi la itikadi kali.
Mahakama hiyo imewahukumu Vadim Kobzev, Igor Sergunin na Alexei Lipster, baada ya kukamatwa, Oktoba 2023 na mwezi uliofuata iliwaongeza kwenye orodha rasmi ya "magaidi na wenye itikadi kali."
Sergunin alifungwa miaka mitatu na nusu, Lipster miaka mitano na nusu na Kobzev miaka mitano na nusu.
Navalny, aliyefariki ghafla akiwa gerezani mwezi Februari mwaka uliopita, pia alikutwa na hatia ya kujihusisha na itikadi kali na mashtaka mengine ambayo yote aliyakana.