1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa EU wahimiza mshikamano mbele ya utawala wa Trump

21 Januari 2025

Mawaziri wa fedha wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuwa na mshikamano na msimamo wa pamoja kuelekea uongozi mpya wa Marekani.

https://p.dw.com/p/4pQaR
Wawakilishi wa Umoja wa Ulaya
Mawaziri wa fedha wa EU wakubaliana kuwa na mshikamano mbele ya utawala mpya wa MarekaniPicha: Miguel Riopa/AFP

Mawaziri hao wamekubaliana kwamba uchumi imara katika Umoja wa Ulaya utakaotowa ushindani ni silaha bora ya kupambana na changamoto kutoka Marekani.

Katika kikao chao kisichokuwa rasmi cha chakula cha usiku,mawaziri wa fedha wa  mataifa 27 ya Umoja huo wa Ulaya pia walikubaliana, kwamba mahusiano thabiti na Marekani ni muhimu kwa maslahi ya pande zote mbili Umoja huo wa Ulaya na Marekani.

Trump asaini maagizo kadhaa ya rais

Kadhalika, wengi wa mawaziri hao waliunga mkono kwamba hatua ya kujumuisha masoko zaidi ya nishati itakuwa na manufaa makubwa kwa jumuiya hiyo.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW