Mawaziri wa kigeni wa Ulaya kukutana leo
20 Machi 2023Matangazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba anatarajiwa kuwafahamisha mawaziri wenzake kwa njia ya video kuhusu hali ilivyo sasa.
Mawaziri wa Ulinzi wa Umoja wa Ulaya watashiriki katika mjadala kuhusu mipango ya kuipatia Ukraine dola bilioni 2, kwa ajili ya kupeleka haraka makombora Ukraine.
Wanadiplomasia hao wanatarajiwa kuweka vikwazo vipya kwa Iran kutokana na ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya waandamanaji wanaoipinga serikali. Hatua kadhaa zilizochukuliwa na Rais wa Tunisia Kais Saied, ili kuimarisha mamlaka yake pia ni ajenda itakayojadiliwa leo.