Mawaziri wa mambo ya kigeni EU wajadili kuhusu amani Libya
20 Januari 2020Hali hiyio imejitokeza baada ya wahamiaji wengi kuingia katika mataifa ya Umoja wa Ulaya na kusababisha na ujumbe huo ulisitishwa mwaka jana wakati ulipozuka mjadala mkali wa wahamiaji.
Mazungumzo hayo mjini Brussels yanakuja masaa kadhaa baada ya mkutano kuhusu Libya mjini Berlin ambamo viongozi wa kimataifa wameahidi kuimarisha vikwazo vya silaha vya Umoja wa Mataifa na kufikisha mwisho usaidizi wa kijeshi kwa makundi ya nchi hiyo yanayopigana.
Waziri mkuu wa nchi hiyo anayekabiliwa na matatizo Fayez al-Serraj anaungwa mkono na Umoja wa mataifa pamoja na uwepo wa majeshi ya Uturuki, wakati kamanda hasimu wake Khalifa Haftar anaungwa mkono na Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu na Urusi.
Libya imekuwa katika machafuko tangu kuondolewa madarakani mwaka 2011 kwa kiongozi wa muda mrefu Moamar Gaddafi na imekuwa uwanja wa mapambano kwa majeshi hasimu ya mataifa ya kigeni. Suala hilo linaonekana kuwa muhimu katika usalama wa Umoja wa Ulaya, baada ya nchi hiyo ya Afrika kaskazini kuwa lango kuu la wahamiaji wanaojaribu kufika barani Ulaya.
Katika mkutano wa jana Jumapili , Umoja wa Ulaya uliahidi kusaidia kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa , ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kutuma vikosi vya jeshi chini ya bendera ya Umoja wa Ulaya.
Doria ya Sophia
Mataifa wanachama ambao hawajawahi kukubaliana juu ya njia ya kupiga hatua kuhusu Libya, wanapaswa sasa kuamua njia bora ya kuchangia wanajeshi watakaotumika kuangalia makubaliano ya kusitisha mapigano na kuheshimiwa kwa vikwazo vya silaha.
Hii inaweza kujumuisha kuanzishwa upya kwa doria za jeshi la majini katika bahari ya Mediterania chini ya operesheni iliyojulikana kama Sophia, ikiwa kimsingi ni ujumbe wa Umoja wa Ulaya wenye lengo la kuzuwia usafirishaji haramu wa binadamu na kulinda utekelezaji wa vikwazo vya silaha dhidi ya Libya.
Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema kabla ya mazungumzo ya leo kuwa, kusitisha mapigano kunahitaji uangalizi:
"Kuna uwezekano aina kadhaa ya kadhaa , lakini usitishaji mapigano unahitaji uangalizi. Huwezi kusema, haya ni makubaliano ya kusitisha mapigano na baadaye unayasahau. Kuna udhibiti wa silaha, na udhibiti wa vikwazo vya silaha. Kuna aina nyingi ya uwezekano, na mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya wanapaswa kuamua cha kufanya ili kusaidia utekelezaji wa makubaliano ya mkutano wa jana wa Berlin kuhusu Libya."
Jana waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Heiko Maas ameelezea hali mbaya yanayokumbana nayo wahamiaji katika makambi nchini Libya. Siwezi kusema kuwa naiangalia hali ya wahamiaji kuwa kinyume na ubinadamu, na kisha nikubaliane kuwa watu warejeshwe huko. Tunapaswa kuzungumza tena juu ya operesheni Sophia bila shaka," aliiambia televisheni ya taifa ARD. Waziri wa mambo ya kigeni wa Italia Luigi Di Maio amesema jana kuwa Italia iko tayari kuchukua jukumu la mbele katika kuangalia amani nchini Libya.