SiasaMarekani
Marekani, Urusi wajadili kupunguza hatari za kusambaa mzozo
13 Julai 2024Matangazo
Wizara za ulinzi za nchi hizo zimearifu kwamba kwenye mazungumzo hayo ambayo Pentagon imethibitisha yaliratibiwa na Moscow, Austin na Belousov walijadiliana juu ya kupunguza hatari ya kile walichosema "uwezekano wa kusambaa" kwa mvutano katikati ya ongezeko la wasiwasi kati ya mataifa hayo mawili, baada ya Urusi kuivamia Ukraine.
Mazungumzo hayo, yanafanyika siku mbili tu baada ya Marekani kutangaza itapeleka makombora ya masafa marefu nchini Ujerumani kwa mara ya kwanza baada ya miaka 20.
Mjini Washington, Naibu msemaji wa Pentagon Sabrina Singh aliwaambia waandishi wa habari kwamba "waziri alisisitiza umuhimu wa kudumisha njia za mawasiliano katikati ya vita vinavyoendelea vya Urusi dhidi ya Ukraine."