May aahidi kufanikisha Brexit
4 Oktoba 2017Amedokeza pia kwamba anataka mazungumzo ya kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya , Brexit yafanikiwe.
Katika hotuba aliyoitoa katika mkutano mkuu wa chama ambayo ilijaa lugha ya kinadharia na kuingiliwa kati na mtu wa kufanya masihara, May amesema kampeni ya uchaguzi ilikuwa "kama imeandikwa, na iliyoelekea katika hali ya urais zaidi."
"Niliongoza kampeni , na nawataka radhi ," amesema.
Wahafidhina wamekasirika baada ya uchaguzi wa mapema wa mwezi Juni ulioitishwa miaka mitatu kabla kwa matumaini ya kuimarisha wingi katika chama chake bungeni, lakini uchaguzi huo ulishuhudia serikali ya May ikipungukiwa wingi.
Matokeo hayo mabaya yamemdhoofisha May na anahangaika kuleta umoja katika serikali yake kuhusiana na masuala ya Brexit na kadhalika.
May amesema.
"Chama cha kihafidhina kinapaswa kuahidi kurejesha ndoto ya Waingereza katika nchi hii kwa mara nyingine tena."
Mazungumzo ya Brexit
Serikali ya Uingereza inataka majadiliano ya Brexit yafanikiwe lakini inajitayarisha pia na hali ambayo yanaweza kushindwa, waziri mkuu Theresa May amewaambia wanachama wa chama chake cha Conservative katika mkutano wa mwaka leo.
"Naamini ni kwa maslahi kila mmoja wetu kwa majadiliano hayo kufanikiwa lakini nafahami kwamba baadhi wana wasi wasi iwapo tuko tayari itakapotokea kwamba yatashindwa. Ni wajibu wetu kama serikali kujitayarisha kwa hilo," May amesema.
"Wakati wapinzani wetu wanakumbatia sera za mambo ya kigeni za kati kwa kati na kujitayarisha kupambana. Baadhi ya watu wanasema tumetumia muda mrefu kuzungumzia maisha ya zamani ya Jeremy Corbyn. Kazi yetu ya kwanza muhimu sana ni kufanikisha Brexit. watu wameamua, tumechukua maelekezo yao. Uingereza inajitoa kutoka Umoja wa Ulaya Machi 2019."
May amefunga mkutano huo wa mwaka wa chama chake kwa hotuba akiwaambia mawaziri wake kujiweka na kulenga katika maisha ya kawaida ya wafanyakazi. katika juhudi za kuwavutia wapiga kura wenye kipato cha chini na kati , May ameahidi kuweka ukomo wa bei na malipo kwa ajili ya nishati na kuifanya serikali irejea katika shughuli za ujenzi wa nyumba kwa ajili ya wananchi.
Alikuwa akizungumza , siku moja baada ya bunge la Umoja wa Ulaya kwa kauli moja kuunga mkono hoja inayoyotoa wito wa mazungumzo ya kibiashara na Uingereza kucheleweshwa kwasababu mazungumzo hayajapiga hatua ya kutosha.
Bunge la ulaya mjini Strasbourg limeishambulia serikali ya May , likisema mivutano ya ndani katika baraza lake la mawaziri inazuwia mazungumzo na masuala muhimu ya kutengana ikiwa ni pamoja na fedha zinazopaswa kulipwa na Uingereza kwa ajili ya kujitoa.
Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe / ape
Mhariri: Idd Ssessanga