1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo kati ya Uingereza na Iraq kuashiria 'enzi mpya'

14 Januari 2025

Mazungumzo hayo yametajwa na Iraq kuwa hatua ya kuashiria enzi mpya ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

https://p.dw.com/p/4p8Hz
Uibngereza Londo | Waziri Mkuu Starmer
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer atamkaribisha Waziri Mkuu wa Iraq Mohammed Shia Al-Sudan mjini London kwa mazungumzo.Picha: Zoe Katzayiannaki/DW

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer atakuwa mwenyeji wa kiongozi wa Iraq Mohammed Shia al-Sudani leo Jumanne kwa mazungumzo kuhusu biashara, usalama na uhamiaji.

Mazungumzo hayo yametajwa na Iraq kuwa hatua ya kuashiria enzi mpya ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Ziara ya Waziri Mkuu huyo wa Iraq mjini London, ambapo pia atakutana na mfalme Charles III, inafanyika zaidi ya miaka 20 tangu Uingereza iliposhiriki katika uvamizi nchini Iraq ulioongozwa na Marekani.

Soma pia: Uingereza kuwawekea vikwazo mawaziri wawili wa Israel

Ofisi ya Waziri Mkuu Starmer imesema ziara hiyo pia itahusisha mazungumzo kuhusu makubaliano ya kurejesha wahamiaji raia wa Iraq wanaoishi nchini Uingereza kwa njia zisizo halali.

Viongozi hao pia watazindua kifurushi cha mauzo ya nje chenye thamani ya pauni bilioni 12.3 ili kuongeza fursa kwa biashara za Uingereza.