Mazungumzo magumu yamkabili Merkel kuunda serikali
25 Septemba 2017na changanmoto kubwa ni kwamba uungwaji mkono wa siasa kali za mrengo wa kulia unapata nguvu.
Angela Merkel ameondoa uwezekano wa kuunda serikali yenye wingi mdogo bungeni baada ya uchaguzi wa Jumapili, lakini alikataa kusema iwapo anatarajia kuunda serikali mpya ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
"Nina nia kwamba tunapaswa kupata serikali imara nchini Ujerumani," Merkel amesema katika mkutano maalum uliooneshwa moja kwa moja katika televisheni kuhusiana na hali baada ya uchaguzi unaowashirikisha viongozi wa vyama vilivyopata nafasi ya kuingia bungeni, unaojulikana kama "mkutano wa tembo".
Badala yake chama cha Merkel cha Christian Democratic CDU na chama ndungu cha jimbo la Bavaria cha Christian Social Union , CSU wanalazimika kufanya majadiliano upya , kuingia katika muungano wa pande tatu kufuatia vyama hivyo vya CDU na CSU kupungukiwa zaidi ya asilimia 8 katika kura walizopata.
Hii itakuwa na maana mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto na walinzi wa mazingira chama cha Kijani na kile kinachopendelea biashara cha Free Democrats FDP baada ya mshirika wake wa serikali iliyopita chama cha Social Democrats SPD kuporomoka na kupata asilimia 20.7 tu, ikiwa ni kiwango cha chini kabisa tangu vita vikuu vya pili vya dunia.
Wapiga kura waliokimbilia AfD
Lakini matokeo ya uchaguzi wa Jumapili pia yana maana vyama vya CDU - CSU vitalazimika kuwarejesha wapiga kura wake ambao wamehamia katika chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Alternative for Germany , chama mbadala kwa Ujerumani AfD, kwa kusikiliza kero zao na wasi wasi wao na kimsingi kuendesha siasa safi, kama alivyosema Merkel wakati akiwahutubia wafuasi wa chama hicho.
"Ni dhahiri kwamba tunakabiliwa na mtihani mgumu, chama cha AfD kuingia bungeni. Tutafanya tathmini ya kina kwasababu tunataka kuwaresha wapiga kura wa AfD kwa kutatua matatizo yao na wakati mwingine wasi wasi wao , lakini pamoja na yote kwa kutumia siasa safi."
Muungano wa vyama pamoja na FDP na chama cha kijani utakuwa na wingi mdogo bungeni wa viti 382 katika bunge la taifa Bundestag lenye jumla ya wabunge 700. Chama cha AfD ambacho kiliasisiwa mwaka 2013 , chama kinachopinga Uislamu, kinachopinga Umoja wa Ulaya na chenye shaka kuhusiana na mabadiliko ya tabia nchi, chama hicho sasa kimejitokeza kuwa changamoto kuu inayoikabili Ujerumani baada ya vita , kikiwa na wabunge zaidi ya 90 baada ya kupata asilimia 13 ya kura.
Kiongozi wa chama cha kijani Katrin Goring-Eckardt ameonya kwamba mazungumzo ya kuunda serikali mpya inayojulikana kama Jamaica kutokana na rangi za vyama hivyo kufanana na bendera ya Jamaica, ikiongozwa na Merkel yatakuwa magumu. "Sisi sio washirika rahisi," amewaambia waungaji mkono wa chama hicho. Lakini Merkel atahitaji washirika kuunda serikali.
Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae
Mhariri: Zainab Aziz