Mazungumzo ya amani katika ukanda wa Gaza yakwama
6 Machi 2024Hii ni baada ya Marekani kusema mazungumzo ya mapatano mjini Cairo nchini Misri sasa yamo mikononi mwa kundi hilo.
Katika taarifa, kundi hilo limesema kuwa limeonyesha kuwa tayari kufikia hali ya kukomesha kikamilifu uchokozi dhidi ya watu wake lakini Israel bado inakwepa masharti yake ya makubaliano.
Soma pia: Juhudi za kusitisha mapigano Ukanda wa Gaza zaendelea
Akilitaka kundi hilo la Hamas kukubali masharti yaliyopo mezani, Rais wa Marekani Joe Biden, alisema jana kwamba Israel inatoa ushirikiano na pendekezo mwafaka lilikuwa limetolewa kwa ajili ya kusitisha mapigano kwa kubadilishana na kuachiwa huru kwa mateka wa Israel.
Hamas imeahidi kuendelea kushiriki katika mazungumzo hayo ya Cairo, lakini maafisa wake wamesema lazima kuwa na usitishaji mapigano kabla ya kuachiliwa kwa mateka wa Israel na kwamba lazima Israel iondoke Gaza na wakazi wote wa Gaza kuweza kurejea katika makazi yao waliyolazimishwa kuyakimbia.