Kiongozi wa walio wengi bungeni nchini Kenya Kimani Ichungwa anatarajiwa kuwasilisha mswada wa kamati ya pande mbili za Azimio la Umoja na Kenya Kwanza kuhusu kubuniwa tena kwa tume ya uchaguzi na mipaka. Hili ni suala moja kati ya masuala mengi yalioibuliwa na upinzani kushirikishwa katika mazungumzo kati ya pande hizo mbili. Mchambuzi wa kisiasa Martin Oloo anachambua kutoka Nairobi