1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Mazungumzo ya kusitisha vita Gaza kufanyika tena Jumapili

16 Machi 2024

Mazungumzo yaliyokwama ya kusitisha vita kati ya Israel na Hamas yanatarajiwa kuanza tena nchini Qatar kesho Jumapili.

https://p.dw.com/p/4dnvm
Raia wa Palestina wakiendelea na zoezi la uokoaji kufuatia uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya anga ya Israel Khan Yunis
Raia wa Palestina wakiendelea na zoezi la uokoaji kufuatia uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya anga ya Israel Khan YunisPicha: Ahmad Hasaballah/Getty Images

Hayo yatakuwa ni mazungumzo ya kwanza yasio ya moja kwa moja kati ya maafisa wa Israel na viongozi wa Hamas tangu kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Wapatanishi wa kimataifa walitarajia kufikia makubaliano ya kusitisha vita kwa muda wa wiki sita kabla ya kuanza kwa mfungo wa Ramadhan mapema wiki hii, lakini Hamas walikataa mpango wowote ambao haungehusisha usitishaji wa kudumu wa vita katika ukanda wa Gaza, ombi ambalo Israel ilikataa.

Soma pia: Israel yatuhumiwa kuwaua watu 20 waliokuwa wakisubiri msaada 

Katika siku za hivi karibuni, pande zote hizo; Israel na Hamas, zimechukua hatua zinazolenga kurudi tena katika meza ya mazungumzo.

Kwa mujibu wa maafisa wa Misri, mazungumzo hayo yanatarajiwa kuanza tena kesho Jumapili lakini yanaweza pia kusogezwa mbele hadi siku ya Jumatatu.