1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya nyuklia huenda yakasimama kwa muda

11 Machi 2022

Mkuu wa Sera za kigeni wa umoja wa ulaya Josep Borrell amesema mazungumzo yanayoendelea juu ya makubaliano ya nyuklia ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani yanahitaji mapumziko ya muda.

https://p.dw.com/p/48Mtg
Österreich | Atomgespräche mit dem Iran
Picha: EU Delegation in Vienna/Handout/AFP

Matamshi ya Josep Borrell yanajitokeza kama ramani iliyoonekana kuwa karibu kwa Marekani kujiunga tena na makubaliano ambayo ilijiondoa yenyewe mwaka 2018 na kwa Iran kupunguza urutubishaji wa kasi wa madinu ya urani unaoendelea katika mpango wake wa nyuklia.

Ingawa Borrell hakufafanua zaidi, kauli hii inajiri wakati Urusi ilikwamisha mazungumzo yanayoendelea kutokana na vikwazo ilivyowekewa kuhusu uvamizi wake nchini Ukraine.

Kupitia mtandao wa twitter Borell amesema yeye kama mratibu, atafanya kazi pamoja na timu yake, kuendelea kuwasiliana na washiriki wote wa mpango wa pamoja wa utekelezaji unaojulikana kama JCPOA na Marekani ili kuondokana na hali ya sasa na kufikia makubaliano.

Akijibu kauli ya Borrell, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Saeed Khatibzadeh amesema kusitisha mazungumzo hayo kunaweza kuwa msukumo wa kusuluhisha suala lolote lililosalia na hakuna ushawishi wowote au uingiliaji kutoka nje utakaoathiri nia yao ya kufikia makubaliano ya mwisho.

Jen Psaki, Msemaji wa Ikulu ya White House amesema kwa mtazamo wao makubaliano yanakaribia kuafikiwa.

Belgien Der Vertreter der Europäischen Union für Außen- und Sicherheitspolitik Josep Borrell
Mkuu wa sera za Kigeni wa Umoja Wa Ulaya Josep BorrellPicha: Dursun Aydemir/AA/picture alliance

Pia sote tunajua kwa kuwa tumepitia mazungumzo haya hapo awali na kwamba mwisho wa mazungumzo kila mara ni wakati huwa sehemu ngumu na yenye changamoto , kwa hivyo nisingefanya tathmini hiyo au kurudia hilo kutoka hapa. Tunaendelea na mazungumzo haya ya kidiplomasia. Ni kwa maslahi yetu sote kukaa kwenye meza ya mazungumzo na ndivyo mpango wetu tutakavyofanya kutoka hapa."Iran: Mazungumzo ya nyuklia yamefikia hatua muhimu

Hata hivyo, Iran imekuwa makini katika mazungumzo ili kutoikasirisha Urusi, ambayo inaiona kama mshirika dhidi ya Marekani. Iran pia ilishirikiana na Urusi nchini Syria kumuunga mkono Rais Bashar Assad. Lakini kutoaminiana kwa kihistoria kati ya mataifa haya mawili pia kupo hasa baada ya Urusi kuivamia Iran wakati wa Vita vya Pili vya Dunia na baadaye kukataa kuondoka.

Lakini wiki iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov alisema alitaka hakikisho angalau katika ngazi ya uwaziri wa nchi kwamba vikwazo vya Marekani havitaathiri uhusiano wa Urusi na Iran. Kauli ambayo ilibua mashaka kuhusu juhudi za miezi kadhaa za mazungumzo yaliyofanyika kurejesha makubaliano ya 2015, ambayo yalishuhudia Iran ikikubali kwa kiasi kikubwa kupunguza urutubishaji wake wa madini ya urani ili kuondolewa vikwazo vya kiuchumi.

Mjumbe wa China katika mazungumzo hayo anasema anasikitishwa na kusitishwa kwa mazungumzo hayo.