1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mbivu au mbichi kwa Rais Trump

18 Desemba 2019

Rais Donald Trump wa Marekani yupo katika kitisho cha kuwa rais wa 3 wa Marekani kushitakiwa pale ambapo baraza la wawakilishi la Marekani likijiandaa kupiga kura ya kihistoria ambayo itafungua milango ya mashitaka yake.

https://p.dw.com/p/3Uzvo
US-Präsident Donald Trump
Rais Donald Trump wa MarekaniPicha: Getty Images/AFP/B. Smialowski

 

Idadi kubwa ya watu wenye kushikizia hatua ya mashitaka dhidi ya Trump imeandamana katika miji kadhaa ikiwemo New York, Boston, New Orleans, Ohio na Los Angeles. Mary Bethi Pringle ni miongoni mwa waandamanaji. " Nnaomba, tusipoteze matumaini ya demokrasia yetu pamoja na yote haya." Carol Rose ni mkurugenzi wa asasi moja ya kiraia mjini Massachusette "Usiku huu tuna maandamano, katika maeneo mengi ya Marekani, ya kuunga mkono Baraza la Wawakilishi kuunga kuvipigia kura vufungu vya ridhaa ya kumshitaki Trump, kwa sababu hakuna aliye juu ya sheria."

Rais Trump aandika barua kali kwa Spika Pelosi

US-Präsident Donald Trump
Rais Donald Trump wa MarekaniPicha: Getty Images/AFP/B. Smialowski

Awali, Rais Trump alisema amewekwa katika mazingira ya jaribio la mapinduzi na mashitaka ya kichawi. Katika barua yake ya kurasa sita, rais huyo alimwambia Spika wa Baraza la Wawakilishi wa chama cha Democratic, NancyPelosi kwamba historia itamuhukumu vikali. Barua hiyo ilitolewa ikiwa muda mfupi tu, baada ya Pelosi kutangaza kwamba baraza la wawakilishi litapiga kura leo hii.

Akiwasilisha ujumbe kwa wenzake wa chama cha Democratic, Pelosi alisema Baraza la Wawakilishi litatumia moja ya mamlaka muhimu sana ambayo limepewa kikatiba wakati wabunge watakapopiga kura kuidhinisha vifungu viwili vya mashtaka dhidi ya rais wa Marekani. Aidha aliongeza spika huyo kwamba katika kipindi hicho muhumi katika historia ya taifa hilo, lazima wabunge wailinde katiba ya nchi dhidi ya maadui wote wa nchi na ndani ya Marekani.

Kiini cha mashitaka ya Trump

Rais Trump anakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka kwa kuiagizia Ukraine kumchunguza makamo wa rais wa zamani wa Marekani Joe Biden, ambae anaongoza katika kinyang'anyiro cha kuwania urais kwa upande wa chama cha Democratic, ikitajwa kuwa kama hatua ya kumpinga katika kuwania urais katika uchaguzi wa 2020 wa Marekani. Trump pia anakabiliwa na shitaka la kufanya njama za kuvuruga uchunguzi wa bunge dhidi yake katika tuhuma hiyo kwa kuwazuia maafisa kutoa ushahidi wao pamoja na kuficha baadhi ya nyaraka. Vifungu viwili vya mashitaka vinatarajiwa kupitishwa na Baraza la Wawakilishi ambalo linadhibitiwa na chama cha Democratic. Kama mchakato utakwenda kama inavyotarajiwa kesi yake itafunguliwa Januari mwakani.