Mchezo wa Karandinga wa DW umerejea
Mchezo wa Karandinga wa DW umerejea
Ushindi wa Kazi
Timu ya LbE Kiswahili: Fundi mitambo, Michael Springer (Kushoto), Grace Kabogo (katikati) mtayarishaji na mwandaaji wa vipindi vya Noa Bongo-Jenga Maisha Yako na Simon John (kulia) mtayarishaji msaidizi, waliofanikisha kurekodiwa mchezo mpya wa ''Karandinga'', hadithi nne kuhusu upelelezi katika Uhalifu wa Mtandaoni, Unyanyasaji wa Majumbani, Uchafuzi wa Mazingira na Biashara Haramu ya Binaadamu.
Kuandaa maandamano
Baadhi ya sehemu za mchezo zinahitaji waigizaji wengi sana studio. Katika hadithi ya ''Unania Taratibu'' kwenye mchezo wa Uchafuzi wa Mazingira, wakaazi wa mji wa Donge la Maji wanaingia mitaani wakitaka kashfa ya uchafuzi wa mazingira katika mji huo, ishughulikiwe kisheria.
Kupambana na uhalifu ni kazi ngumu
Kesi na njama mpya, mashujaa na wabaya wapya. Katika mchezo yetu mipya Katika mchezo wa Uhalifu wa Mtandaoni ''Bonyeza Kiunganishi'', maafisa wa polisi wanachunguza tukio la kuchomwa kisu mwanafunzi wa kike wa chuo.
Uhalisia wa mchezo
Uigizaji wa redio una zaidi ya sauti moja. Katika hadithi ya ''Unania Taratibu'' kwenye mchezo wa Uchafuzi wa Mazingira, kiwanda cha chuma kinatumia madini ya risasi ambayo ni hatari kwa maisha ya binadamu pamoja na mazingira. Mmoja wa wafanyakazi anakufa kutokana na sumu hiyo kwa sababu ya kukosa vifaa vya kujikinga akiwa kazini. Mtoto wa mfanyakazi mmoja pia anaugua.
Kubakia salama mtandaoni
Katika mchezo wa Uhalifu wa Mtandaoni ''Bonyeza Kiunganishi'', Mohamed Kaboba aliyecheza kama Tembo, mtalaamu wa IT anamsaidia Rachel Kubo aliyeigiza kama Kendi, kuhusu shughuli za mtandaoni. Pia anamuonya kuhusu hatari inayoweza kujitokeza wakati anatumia mtandao wa Intaneti na mitandao ya kijamii.
Maandalizi ya mwisho
Kati ya kila tukio, huwa kuna muda wa kupumzika na kupitia hadithi zinazofuata. Pichani ni Mwasiti Hussein aliyeigiza kama Samira na Rachel Kubo aliyeigiza kama Ramatu, mwanafunzi kijana aliyejitolea kupigania haki za wanawake, katika mchezo wa ''Chozi la Mnyonge''
Furaha Studio
Katika hadithi ya ''Jinamizi la Mauaji'' kwenye mchezo wa Biashara Haramu ya Binadamu, polisi wanajaribu kutafuta ukweli kuhusu kifo cha mhudumu kijana katika mgahawa mmoja, ambaye utambulisho wake bado ni siri.
Vijana wabaya au vijana wazuri?
Inategemeana na hadithi, waigizaji wanaweza wakacheza nafasi tofauti. Katika mfululizo wa mchezo wa Karandinga, Hassan Kazoa na Macray Rusasa wanaonyesha jinsi ambavyo wanaonekana wema, ilhali katika mchezo wameigiza kama wauzaji wa watu katika hadithi ya ''Jinamizi la Mauaji'' kwenye mchezo wa Biashara Haramu ya Binadamu.
Onyo! Uhalifu
Katika hadithi ya ''Jinamizi la Mauaji'' kwenye mchezo wa Biashara Haramu ya Binadamu, Kodjo Dagata, nafasi iliyochezwa na Aloyce Michael, ana ndoto za kuwa na maisha bora baadae katika nchi jirani. Rafiki yake anamuahidi kupata fusra za mafunzo mazuri. Lakini hali halisi inamsubiri akifika huko.
Furaha ya ushindi
Timu ya waandamaji wa LbE na baadhi ya waigizaji wakifurahi baada ya kukamilisha kazi ya kurekodi michezo yote ya LbE jijijini Dar es Salaam, Tanzania. Ingawa kwa kawaida kabla ya kuanza kurekodi, waigizaji wanapaswa wapitie nafasi zao za kuigiza, ambapo katika mchezo wa ''Chozi la Mnyonge'' kuhusu Unyanyasaji wa Majumbani, Samira, anageuka kuwa afisa wa polisi, baada ya kunyanyaswa na mumewe.