Mchimbaji apatikana hai wiki nzima baada ya kufukiwa mgodini
6 Desemba 2023Miili ya watu wawili pia ilipatikana kutoka kwenye vifusi vya mgodi huo wa mkoa wa Copperbelt wa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.
Maafisa wa serikali wamesmea zaidi ya wachimba madini 30 huenda bado wamekwama chini ya ardhi, ijapokuwa hawajathibitisha idadi kamili.
Kwa mujibu wa Idara ya Kuyashughulikia Majanga nchini Zambia, mtu huyo mwenye umri wa miaka 49 aliokolewa jana usiku.
Soma zaidi: Hichilema bado ana matumaini kupatikana wachimba madini 25
Aliwaambia waokoaji kuwa alitatizika kwa siku tano kutafuta njia ya kuondoka mgodini hapo karibu na mji wa Chingola.
Rais Hakainde Hichilema alisema bado ana matumaini kuwa wachimba migodi hao bado wako hai.
Juhudi za uokoaji zinaendelea wakati timu za uokoaji wakiwemo wanajeshi na makampuni mengine makubwa yakichukuwa tahadhari kutokana na utelezi unaopunguza kasi ya operesheni hiyo