1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mexico City. Kimbunga Wilma chashambulia Cuba na Mexico.

24 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEPA

Kiasi cha watu wanane wameuwawa katika pwani ya Caribik ya Mexico kutokana na kimbunga wilma. Kimbunga hicho kinatarajiwa kushambulia pwani ya Marekani leo Jumatatu, kikiwa na upepo unaokwenda kasi ya karibu kilometa 160 kwa saa.

Nchini Cuba ambako upepo mkali na mvua kubwa vinaendelea kushambulia , imewaondoa wakaazi zaidi ya 630,000 kutoka katika wilaya zilizoko katika maeneo ya pwani yaliyoko katika njia inayopitia kimbunga hicho Wilma.

Serikali ya Bahamas pia imetoa tahadhari kuhusu kimbunga hicho katika maeneo yake ya kaskazini magharibi.

Maafisa wa Florida wameamuru watu 80,000 wakaazi wa visiwa vya Florida Keys kuondolewa kwa lazima. Licha ya wito wa gavana wa jimbo hilo Jeb Bush , wakaazi wengi wamepuuzia wito huo.

Eneo la kusini la Marekani limekwisha shambuliwa na vimbunga vinne mwaka huu. Kimbunga Rita kilisababisha zaidi ya watu 1,200 kupoteza maisha yao katika ghuba ya Mexico nchini Marekani.