JangaMexico
Mexico yaomba mkutano wa kukabili tatizo la wahamiaji
28 Septemba 2023Matangazo
Lopez Obrador amesema hilo si suala linaloisumbua Mexico tu bali ni suala la kimfumo linalotakiwa kushughulikiwa kwa jinsi hiyo. Amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari na kuongeza kuwa anatarajia pengine mkutano huo utafanyika katika kipindi cha siku kumi zijazo.
Amesema kuna haja ya kuwa na mpango wa pamoja, akiangazia ulinzi wa wahamiaji pamoja na udhibti wa vyanzo vinavyowasukuma watu ambao wengi wao wanatokea Venezuela, Cuba na mataifa ya Amerika ya Kati kuondoka makwao.
Idadi kubwa ya wahamiaji wamekuwa wakivuka na kuingia Marekani wakitokea Mexico katika wiki za karibuni, na kuongeza shinikizo kwa serikali ya rais Joe Biden juu ya kudhibiti hali hiyo.