1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mexico yapata rais wa kwanza mwanamke

Josephat Charo
2 Oktoba 2024

Claudia Sheinbaum ameapishwa kuwa rais wa kwanza mwanamke wa Mexico siku ya Jumanne (Oktoba 1).

https://p.dw.com/p/4lKEz
Rais mpya wa Mexico, Claudia Sheinbaum.
Rais mpya wa Mexico, Claudia Sheinbaum.Picha: Alfredo Estrella/AFP/Getty Images

Sheinbaum anarithi nchi inayokabiliwa na machafuko ya magenge na kutokuwa na uhakika wa kiuchumi kuhusiana na mageuzi yenye utata yaliyopitishwa na chama chake tawala chenye nguvu.

Meya huyo wa zamani wa mji mkuu, Mexico City, mwenye umri wa miaka 62, alikula kiapo cha kushika wadhifa huo bungeni, huku viongozi wa kigeni wakishuhudia, akiwemo mke wa rais wa Marekani, Jill Biden.

Soma zaidi: Rais wa Mexico awasilisha ripoti kuhusu utendaji wa serikali yake

Sheinbaum aliwaambia wabunge waliokuwa wakishangiliwa kwamba, kwa mara ya kwanza, wanawake wamefika ili kutengeneza hatima ya taifa lao zuri, ambapo takriban wanawake au wasichana 10 huuwawa kila siku.