Wataalamu wetu wanaijadili hali ya nchini Gabon baada ya wanajeshi wa nchi hiyo kufanya mapinduzi na kutwaa mamlaka.
Kiongozi wa wanajeshi hao jenerali Brice Oligui Nguema ameshaapishwa na ameahidi kurejesha utawala wa kiraia kwa njia ya uchaguzi huru, wa kuaminika na wa uwazi. Je, mapinduzi hayo yataleta neema kwa watu wa eneo hilo au ni pigo dhidi ya demokrasia?