1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfalme Charles: Historia "chungu" ya utumwa ikumbukwe

Angela Mdungu
25 Oktoba 2024

Mfalme Charles wa Uingereza amesema Jumuiya ya Madola inapaswa kutambua historia yake "chungu" kuhusu utumwa.

https://p.dw.com/p/4mDo2
Ziara ya Kifalme ya Australia na Samoa | Mfalme Charles III
Ziara ya Kifalme ya Australia na Samoa, Mfalme Charles III akipewa kinywaji cha 'Ava' wakati wa makaribisho rasmi huko Australia na Samoa October 24, 2024. Picha: Chris Jackson/PA/empics/picture alliance

Kauli hiyo ameitoa wakati mataifa ya Kiafrika na Karibiani yakizidi kushinikiza kulipwa fidia juu ya jukumu la Uingereza katika biashara ya utumwa wa Bahari ya Atlantiki. Wawakilishi wa nchi 56, wengi wao wakiwa na mizizi katika himaya ya Uingereza, wanahudhuria Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola ulioanza nchini Samoa siku ya Jumatatu. Mkutano huo umegubikwa na historia ya masuala ya utumwa na mabadiliko ya tabia nchi.Charles hata hivyo hakugusia suala la fidia za kifedha zinazoshinikizwa na viongozi katika mkutano huo, na badala yake akahimiza kutafuta "lugha sahihi" na uelewa wa historia.