1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAustralia

Mlezi wa zamani wa watoto awanyanyasa watoto 91, Australia

1 Agosti 2023

Mfanyakazi mmoja wa zamani wa kulea watoto nchini Australia ameshitakiwa kwa kuwanyanyasa watoto 91 katika kile polisi imeeleza kuwa moja ya kesi za kutisha zaidi za unyanyasaji wa watoto kingono nchini humo.

https://p.dw.com/p/4Ucdh
Watoto wasoma vitabu walivyoazima, katika nyumba ya Mohamed Abdel Aziz ambayo imegeuzwa kuwa kituo cha bure cha kujifunzia kwa wanafunzi wa kijijini ambao wanakosa huduma na shughuli za kitamaduni, mjini Cairo nchini Misri
Watoto nchini Misri katika nyumba iliyogeuzwa kuwa kituo cha bure cha kujifunzia kwa wanafunzi wa kijijiniPicha: Mohamed Abd El Ghany/REUTERS

Mwanamume huyo ameshitakiwa kwa visa tofauti 1,623 vya uhalifu, ikiwemo makosa 136 ya ubakaji na 110 ya kufanya ngono na mtoto mdogo wa chini ya umri wa miaka 10. Wapelelezi walimkamata mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 45 baada ya kugundua picha chafu za watoto zilizochapishwa kwenye mtandao wa kihalifu, kwa kutumia vidokezo ambavyo hatimaye viliwasaidia kuwafuatilia watoto hao hadi kituo cha malezi ya watoto mjini Brisbane. 

Picha na video zafichua uzito wa makosa hayo

Lakini ni wakati walipoanza tu kupekua kwenye simu na kompyuta yake ndipo waligundua uzito wa makosa hayo ya kutisha yalioonekana kupitia kwenye picha na video 4,000 walizopata. 

Polisi imesema uhalifu huo ulifanyika katika vituo 1o tofauti vya malezi ya watoto kati ya mwaka wa 2007 na 2022 na haswa uliwalenga wasichana wa kabla ya kubalehe.