1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgogoro wa kisiasa wazidi kutanuka Iraq

23 Agosti 2022

Mahakama nchini Iraq imezisimamisha shughuli zake ikiwa ni baada ya wafuasi wa kiongozi wa kidini mwenye ushawishi mkubwa Moqtada al-Sadr kuongeza shinikizo lake katika kuvunjwa kwa bunge.

https://p.dw.com/p/4FvZZ
Irak Muktada al Sadr
Picha: Ali Najafi/AFP/Getty Images

Hatua hiyo imeelezwa kuwa mgogoro mkubwa tangu uvamizi wa Marekani.

Katika siku za hivi karibuni kiongozi huyo amesababisha uwepo wa hali ya wasiwasi kwa kuamuru maelfu ya wafuasi kuvamia na kudhibiti bunge, na hivyo kuzuia uundwaji wa serikali ikiwa takribani miezi 10 tangu kufanyika kwa uchaguzi.

Waziri Mkuu wa Iraq, Mustafa al-Kadhimi, ambaye amekatisha ziara yake nchini Misri ili aweze kushughulikia mgogoro huo, amezitaka pande zote kuwa tulivu na kurejea wito wake wa mazungumzo ya kitaifa.