Mgombea mwenye msimamo wa wastani kileleni uchaguzi wa Iran
29 Juni 2024Huku zaidi ya kura milioni 3.8 zikiwa zimehesabiwa hadi sasa, Massoud Pezeshkian anaongoza na zaidi ya kura milioni 1,595,000 na mpinzani wake wa msimamo mkali, mpatanishi wa zamani wa mazungumzo ya nyuklia Saeed Jalili akiwa na karibu milioni 1,594,000. Hayo yametangazwa kwenye televisheni na afisa wa wizara ya mamho ya ndani Mohsen Eslami.
Vyanzo vinasema idadi ya wapiga kura waliojitokezailikuwa karibu asilimia 40, ikiwa ni chini kuliko ilivyotarajiwa na watawala wa kidini wa Iran. Shirika la habari la Iran, Tasnim, limesema kuna uwezekano mkubwa wa uchaguzi huo kuingia duru ya pili ili kumpata mrithi wa Ebrahim Raisi aliyekufa katika mkasa wa kuanguka helikopta.
Soma pia: Rais wa Iran amefariki katika ajali ya helikopta
Uchaguzi huo unafanyika sanjari na kuongezeka kwa mvutano wa kikanda kutokana na vita kati ya Israel na washirika wa Iran Hamas huko Gaza na Hezbollah nchini Lebanon, pamoja na kuongezeka kwa shinikizo la Magharibi kwa Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia unaoendelea kwa kasi.