1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 25 baada ya Srebrenica, Mahakama kimataifa zahitajika

Sekione Kitojo
11 Julai 2020

Miaka 25 baada  ya  mauaji  ya  Srebrenica mahakama za kimataifa kama ile iliyowahukumu waliofanya  mauaji zinakabiliwa  na  hali isiyofahamika ya baadaye  lakini zinahitajika  kuliko wakati mwingine, wataalamu wanasema.

https://p.dw.com/p/3f97N
Bosnien und Herzegowina Srebrenica Krieg
Picha: DW/M. Sekulic

Mahakama iliyomaliza muda wake ya uhalifu ambayo  iliwahukumu viongozi wa  Waserb wa  Bosnia kama  Ratko Mladic na  Radovan Karadzic kuhusiana  na  mauaji ya  Waislamu 8,000  wanaume  na  vijana ilisifiwa  katika  wakati  fulani  kama  enzi mpya ya  uwajibikaji  wa  baada  ya  vita  baridi. pamoja  na  hayo mahakama  kadhaa  zilizoundwa  baada  ya  hapo  zinakabiliwa  na matatizo  kadhaa  kama  viwango vya chini  vya  hukumu , mashambulio ya rais wa Marekani Donald Trump pamoja  na  serikali zinazopinga, na  shutuma za  ubaguzi.

Bosnien und Herzegowina Srebrenica
Familia za wahanga wakiwa katika eneo la makaburi ya mauaji ya SrebrenicaPicha: DW/M. Sekulic

Pia  zinahitaji  kuanza  kutoa  haki  kwa  wahanga  wa  uhalifu  wa enzi  hii  mpya  kama  vita  nchini  Syria, kukandamizaji wa  watu  wa jamii  ya  Rohingya  nchini  Myanmar  na  ukandamizaji   dhidi  ya Waiughur wa  China, wataalamu  wanasema.

Kumbukumbu  ya  Srebrenica  ni kumbusho kuwa  haja  ya mahakama  kama  hizo kupambana  na  mauaji  ya  halaiki "ni  kubwa kupita wakati wowote," amesema  Nancy Combs, profesa  wa sheria  katika  chuo  kikuu  cha  sheria  cha  William and mary Law jimboni  Virginia.

The Hague  nchini  Uholanzi , unaofahamika  kama  mji wa "amani  na haki" ni  mwenyeji wa  mahakama  hizi , kubwa  kabisa  ikiwa mahakama  ya  kimataifa  ya  uhalifu, iliyoundwa  mwaka  2002 kuhukumu  matukio  mabaya  kabisa duniani  ya  uhalifu.

Pia  ni mji  ambao  una  mahakama  kwa  ajili  ya  Kosovo ambayo hivi  karibuni  ilitoa mashitaka  ya  uhalifu  wa  kivita  dhidi  ya  rais Hashim Thaci,  na  mahakama  kuhusu  mauaji  ya  waziri  mkuu  wa zamani  wa  Lebanon rafiq hariri  mwaka  2005.

Bildkombo Radovan Karadzic und Dragan Dabic
Mahakama ya ICC iliwahukumu viongozi wa Waserb wa Bosnia Radovan Karadzic na Dragan DabicPicha: picture-alliance/dpa/M. Evstafiev/Healthy Life Magazine

Matatizo dhidi  ya  ICC

Lakini  mahakama  ya  ICC hivi  sasa  inakabiliwa  na  mashambulio dhidi  ya  utawala  wa  Trump kwa  kufanya  uchunguzi  wa  madai ya  uhalifu  wa  kivita  nchini  Afghanistan, wakati utaratibu  wa  haki umegeuka  taratibu  kuwa  kuwa  wa  ghali  kwa  Kosovo  na Lebanon.

Niederlande Den Haag Internationaler Strafgerichtshof | Laurent Gbagbo, ehemaliger Präsident Elfenbeinküste
Rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent GbagboPicha: Reuters/J. Lampen

"Bila  shaka mahakama  hizi zinapitia  katika  nyakati  ngumu  kabisa kwa  sasa," amesema  Combs.

"Katika  wakati  huu katika  historia, hali  ya  baadaye  ya mahakama  za  uhalifu haijulikani."

Mahakama  ya  ICC pia "inapitia  katika  kipindi  cha  mzozo wa imani kwasababu  mafanikio  yake  yamekuwa  madogo  mno katika  kipindi cha  muongo  mmoja  uliopita," Combs  aliliambia  shirika  la  habari la  AFP.

Niederlande Chefanklägerin beim Internationalen Strafgerichtshof in Den Haag | Fatou Bensouda
Fatou Bensouda mwendesha mashitaka mkuu wa ICCPicha: Getty Images/AFP/E. Plevier

Mahakama hiyo  ilibidi  kutupilia  mbali  kesi  ya  uhalifu  dhidi  ya ubinadamu dhidi  ya  rais  wa  Kenya  Uhuru  Kenyatta, wakati  huo huo kumwachia  huru  rais  wa  zamani  wa  Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo  na  mwanasiasa  wa  Jamhuri  ya  Kidemokrasi ya Congo Jean-Pierre bemba  na  kuwa  kama  pigo  kubwa  kwa  mahakama hiyo.

Licha  ya  mabadiliko  ya  hivi  karibuni  nchini  Sudan, kiongozi ambaye  alikuwa  akitafutwa  sana  na  mahakama  hiyo  rais  wa zamani  wa  Sudan Omar al-bashitr bado  hajapatikana na kufikishwa  katika  mahakama  hiyo. Madai  kwamba  ICC ilikuwa  tu inawahukumu watuhumiwa  kutoka  bara  la  Afrika  pia yamesababisha  shutuma  za  ubaguzi.