Miaka 31 ya mauaji ya Tiananmen,maandamano yazuwiwa HongKong
4 Juni 2020China inadumisha ulinzi huko Hong Kong dhidi ya waandamanaji wanaodai demokrasia ambao wanapanga kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 31 tangu wanajeshi kufyatua risasi dhidi ya waandamanaji wanafunzi ndani na nje ya uwanja wa Tiananmen, jijini Beijing. Hiyo inafuatia hatua ya viongozi wa Hong Kong kupiga marufuku maadhimisho kwenye bustani ya Victoria Park kwa sababu ya kuzuwiya maambukizi ya virusi vya Corona.
Kwa mda mrefu, China inachukulia vibaya maadhimisho hayo ya kumbukumbu ya mauwaji ya Tiananmen, ambayo kila mwaka yamefanyika huko Hong Kong. Mamia huenda maelfu ya watu waliuliwa wakati wanajeshi wa China wakisaidiwa na vifaru vya kijeshi waliwafiatulia risasi waandamanaji wa kutetea demokrasia katikati mwa jiji la Beijing usiku wa kuamkia tarehe 4 Juni mwaka 1989. Chama cha Kikomunisti cha watu wa China kimechukuliwa maandamano ya wanafunzi kama tishio la utawala wake.
Baraza la Taifa la Umma wa China lapitisha sheria ya usalama wa taifa
Sote tunafahamu kwamba serikali ya Hong Kong na ile ya China hazitaki kuona mishumaa zimewashwa kwenye bustani ya Victoria Park ilikuadhimisha siku ya kumbukumbu,alisema Wu'er Kaixi,kiongozi wa zamani wa wanafunzi walioandamana huko Tiananmen.Kaixi alikuwa mtu wa pili kwenye daftari ya watu waliokuwa wakitafutwa sana na serikali ya China baada ya maandamano ya mwaka 1989.
Uwanja wa Tiananmen ambako maelfu ya wanafunzi walikusanyika miaka 31 iliopita,ulikuwa kimya na bila msongamano alhamisi.Polisi na vifaru vya kijeshi vilionekeana kwenye uwanja huo. Watu wachache walionekana huku wakifanyiwa uchunguzi wa vitambulisho vyao katika juhudi za kitaifa za kuepusha maandamano.
Kufutwa kwa sherehe za kuwasha mishumaa kumekuja baada shinikizo la Beijing,kupitia Baraza la Taifa la Umma wa China, kutaka HongKong kupitisha sheria mpya kuhusu usalama wa taifa.Sheria hiyo itairuhusu serikali ya Hong Kong kuanzisha vituo vya idara za China bara katika mji huo zitakazowawezesha maafisa wa China kuwakamata watu kiholela watakaposhiriki katika harakati zitakazozingatiwa kuwa za kutetea demokrasia.
Mjini Hong Kong ,sheria hiyo itawahukumu makosa ya ughaini ukosoaji wa wimbo wa taifa wa China. Wanaharakati mashuhuri 15 wa HongKong walikamatwa kwa kupanga na kushiriki kwenye maandamano yasiyo ya kisheria. China bara imekuwa ikitumia mara kwa mara sheria ya kitaifa ya usalama kuwakamata wanaharakati, waandishi wa habari na wanasheria bila ya kuwafungulia mashitaka ama kuwapatia fursa ya kupata mawakili.
Hatua hizo za China zimekwenda kinyume na haki za kiraia za Hongkong zilizoafikiwa kwenye mkataba na Uingereza ,ilipoukabidhi mji huo kwa China mwaka wa 1997.