Agosti mwaka 1968 askari nusu milioni walioongozwa na vikosi vya vifaru vya Umoja wa Kisoviet waliizima ndoto ya watu wa Chekoslovakia ya kuleta mageuzi ya kisiasa, yaliyoitwa Mapambazuko ya Prague. Nchi hiyo na nyingine za Ulaya Mashariki zilikuwamo katika himaya ya Kisoviet baada ya kumalizika vita vikuu vya pili.