Miaka 60 ya Idhaa ya Kiswahili ya DW
Miaka 60 ya Idhaa ya Kiswahili ya DW
Tulikoanzia
Timu ya Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle katika miaka ya 1960, siku hizo ikijuilikana kwa jina la Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani.
DW Kiswahili katika miaka ya 70
Kutoka kushoto, ni Mohammed Abdulrahman na Prema Martin, na kutoka kulia ni Ramadhani Ali na Othman Miraji.
Barua za wasikilizaji wetu!
Wafanyakazi na watangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle wakichagua barua kwenye sanduku la kupokelea barua za wasikilizaji katika miaka ya 1970.
Watangulizi wetu
Timu iliyoikuza DW kufikia hapa ilipo. Watangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW katika ubora wao miaka ya 1980.
Enzi hizo
Hawa ni baadhi ya watangazaji mahiri wa DW waliochangia Idhaa kuvuma kwa kishindo. Sekione Kitojo na Oumilkheir Hamidou ambao sasa ni wastaafu.
Sauti ya dhahabu
Mtangazaji mkongwe aliyepata umashuhuri mkubwa kutokana na sauti yake iliyowakosha wasikilizaji wa DW, Oumilheir Hamidou (kushoto) akiwa kazini na mratibu wa DW Kiswahili Samia Othman.
Mahojiano na watu mashuhuri
Mwaka 2005, mgombea urais wa Tanzania wakati huo, kupitia chama tawala CCM, Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza na DW Kiswahili, siku chache kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu nchini humo.
Karibuni
Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili, Andrea Schmidt (katikati) akiwa na waandishi wa Tanzania walipoitembelea DW Kiswahili.
Tunavuma kwa kishindo!
Kijana huyu anasikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili kupitia redio yake katika mitaa ya jiji la Dar es Salaam.
Miaka 10 nyuma
Kutoka kushoto ni Ramadhan Ali, Prema Martin, Andrea Schmidt( Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili) na Othman Miraji katika maadhimisho ya miaka 50 ya Idhaa ya Kiswahili ya DW 2013.
Tahadhari! sio kila kizu ukisomacho ni sahihi
Wazungumzaji katika kongamano kuhusu taarifa za uzushi mjini Dar es Salaam Tanzania, 2017. Kutoka kushoto ni mwandishi habari mkongwe, Jenerali Ulimwengu; Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC), Ayoub Rioba, mtangazaji wa DW, Kiswahili Mohammed Khelef, Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forums, Maxence Melo na Waziri wa Habari wakati huo, Dk. Harrison Mwakyembe.
Wageni wetu
DW imekuwa ikipokea wageni kutoka maeneo yote ya dunia. Katika picha hii balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dk. Abdalla Posi (wa pili kutoka kushoto), akiambatana na afisa kutoka ubalozi huo Rafael Macha (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili Andrea Schmidt (katikati) Naibu wake Josephat Charo na Mtangazaji wa DW Kiswahili Sudi Mnette (kulia).
DW Kazini
Vipawa huzaliwa, lakini uwezo hujengwa. Abdu Mtullya (kulia) akichangiana maarifa na ujuzi wake na watangazaji wapya, Grace Kabogo (katikati) na Stumai George.
Mkuu wa kwanza wa Kiafrika
Ben Wazir ni miongoni mwa watangazaji wa mwanzo kabisa wa DW Kiswahili na mkuu wa kwanza Mwafrika wa Idhaa hiyo.
Tunakuletea habari za uhakika
Kwa miaka 60 tumekuwa nawe bega kwa bega, tukikupasha habari kutoka nyanja zote za dunia, bila kujali unakotoka. Tunatoa nafasi sawa kwa kila mmoja kuchangia katika matangazo yetu. Studioni ni Josephat Charo (kushoto) na Zainab Aziz.
DW Kiswahili na redio washirika
Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili, Andrea Schmidt (kushoto) akiwa pamoja na watangazaji wa kituo mshirika cha redio Tumaini ya Dar es Salaam inayorusha matangazo yetu kupitia masafa ya FM kwa wasikilizaji wa Tanzania.
Veronica Natalis Arusha, Tanzania
Mwakilishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle kaskazini mwa Tanzania, Veronica Natalis (kushoto), akiwa kazini.
Maigizo ya mchezo wa Noa Bongo Jenga Maisha Yako
Baadhi ya waigizaji wa mchezo mashuhuri wa Karandinga ambao ni sehemu ya maigizo ya kipindi cha Noa Bongo cha DW Kiswahili, wakiwa studioni jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Idhaa ya Kiswahili ya DW 2000
Kutoka kushoto: Halima Nyanza, Thelma Mwadzaya na Andrea Schmidt wakiwa kwenye mkutano wa kupanga matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW mwaka 2009.
Amina Abubakar, DW 2013
Tunaamini katika ufanisi na umakini wa kazi zetu. Amina Abubakar akiwa kazini kwenye studio za DW Bonn
Wakongwe na wapya, DW 2013
DW Kiswahili sio tu kwamba ni redio ya kutangazia wasikilizaji wake, bali pia taasisi ya kuwatayarisha wafanyakazi wake, ambapo wazoefu huchangia mawazo na wanagenzi ili kurithishana ujuzi na maarifa. Samia Othman (kushoto) na Bruce Amani.
Matangazo yakipelekwa hewani
Mti ni nyenzo! Kuifanya sauti ya watangazaji isikike kwenye redio kwa wakati na kwa mpangilio unaostahiki ni kazi kubwa, na nyuma ya kazi hiyo kuna Nina Markgraf (kushoto), muongozaji wetu wa matangazo.
Wabobezi wa fani ya utangazaji
Sauti zilizovuma miaka ya 1990 katika Idhaa ya Kiswahili ya DW wakati huo ikiwa mjini Cologne. DW Kiswahili ilikwenda hewani kwa mara ya kwanza tarehe mosi Februari, 1963
Kizazi cha zamani na Kipya
Kutoka kushoto Samia Othman, Nina Markgraf, Amina Abubakar, Pendo Ndovie, Sudi Mnette, Andrea Schmidt, Salma Saidi, Caro Tsuma, Othman Miraji, Abdu Mtullya, Oumilkheir Hamidou. Waliochuchuma kutoka kushoto ni Sekione Kitojo, Mohammed AbdulRahman, na Daniel Gakuba.
Watangazaji wa sasa
Hii ndio timu ya sasa ya watangazaji wa DW Kiswahili.
Ahsanteni sana!
Mchoro wa Said Michael kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 60 ya Idhaa ya Kiswahili ya DW. Tunawashukuru kwa uaminifu wenu.