1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michuano ya 21 ya Ligi ya Ujerumani

Mohamed Abdulrahman13 Februari 2015

Weder Bremen inacheza nyumbani ikiikaribisha Ausburg, Borussia Monchen gladbach ni wenyeji wa FC Cologne na Hoffenheim inamenyana na Stuttgart ambayo inakamata mkia ikikabiliwa na hatari ya kushuka daraja

https://p.dw.com/p/1EbHP
Siku ya mchuano wa Wolfsburg na Hoffenheim katika ligi ya Ujerumani
Picha: Stuart Franklin/Bongarts/Getty Images

Ama Mabingwa watetezi Bayern Munich wanawakaribisha watani wao wa kaskazini Hamburg. Wakati Bayern ikiwa na matumaini makubwa ya kuendelea kujizatiti kileleni kuhakikisha inautwaa tena ubingwa msimu huu, inapointi 8 mbele ya Wolfsburg ilioko nafasi ya pili na ambayo itakuwa ugenini kuvaana na Bayer Leverkusen. Schalke 04 inayosimama nafasi ya tatu katika matokeo jumla inacheza na Eintracht Frankfurt.

Jumapili Hertha Berlin watacheza na Freiburg , kilabu nyengine inayoandamwa na janga la kushuka daraja sawa na Stuttgart, wakati Hanover itaumana na Paderborn.

Mnyukano katika ligi ya Uhispania

Katika La Liga ,ligi kuu ya Uhispania , Leo Real Madrid inakutana na Deportivo La Coruna, ikiwa ni wiki moja baada ya kipigo ilichokipata kutoka kwa watani wao wa mjini Athletico Madrid cha mabao 4-0 . Athletico wao watakaribishwa na Celta Vigo kesho nayo Barcelona hiyo hiyo kesho itacheza na Levante

Spanien Fussball Club Atlético de Madrid gegen Real Madrid CF
Klabu ya Atlético ilipomenyana na Real MadridPicha: Dani Pozo/AFP/Getty Images

Nchini Uingereza mchezaji wa kimataifa wa Ubeligiji Eden Hazard amesaini mkataba wa miaka mitano na nusu na Chelsea, inayoongoza ligi kuu ya England Premier League. Hazard mwenye umri wa miaka 24 aliyejiunga na Chelsea kutoka Lille ya Ufaransa Juni 2012, ameshacheza mechi 147 akifunga mabao 43 kwa kilabu hiyo ya Chelsea ya mjini London. Hazard aliyetajwa kuwa mchezaji kijana wa mwaka wa Ligi kuu ya England na mchezaji pia wa mwaka wa kilabu hiyo mwishoni mwa msimu uliopita, aliuhitimisha mwaka jana akiwa amepachika mabao 17 katika mashindano yote. Meneja wa Chelsea Jose Mourinho alisema amefurahi kuwa Hazard amesaini mkataba mpya na Hazard akamshukuru Mourinho akisema amemsaidia kuwa bora zaidi na mashabiki na wachezaji wenzake wamempa motisha kwa kiwango kikubwa. Itakumbukwa Hazard aliisaidia Ubeligiji kufika robo fainali ya kombe la dunia , mashindano yaliofanyika nchini Brazil 2014.

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman
Mhariri: Iddi Ssessanga