Migomo nchini Afrika Kusini yaendelea kwa siku ya tatu
29 Julai 2009Matangazo
Wakaazi wa maeneo ya madongo poromoka katika
majimbo kadhaa waliandamana kutaka huduma bora kwa umma, huku
wafanya kazi wa manispaa wakiandamana pia kwa siku ya tatu leo
wakishikilia waongezewe mishahara. Wakati huo huo, wafanya kazi
katika sekta ya viwanda vya kemikali wametangaza kuumaliza mgomo
wao wa siku nane baada ya kupewa nyongeza ya mishahara baina ya
asilimia tisa na kumi. Uchumi wa Afrika Kusini unajionea kwenda chini
sana kuwahi kuonekana tangu mwaka 1992, na vyama vya wafanya
kazi vinasema hali hiyo inawaumiza sana walio maskini.
Othman Miraji alimuuliza kwa njia ya simu mwandishi wa habari Issac Khomu juu ya mgomo wa wafanyakazi wa manispaa, unaendelea vipi?
Mwandishi: Othman Miraji
Mhariri: Mohamed Abdulrahman