SiasaSudan
Miji ya Darfur yashambuliwa huku vita vya Sudan vikisambaa
14 Juni 2023Matangazo
Vita kati ya jeshi na RSF vimesababisha mzozo wa kiutu wa kibinadamu mjini Khartoum, pamoja na miji mingine ikiwemo El Obeid, Nyala, El Fashir na El Geneina, ambako zaidi ya watu 1,100 wameuawa.
Akizungumza na kituo cha televisheni cha Al-Hadath kutokea mji wa El Geneina, huku milio ya risasi na makombota ikisikika, gavana wa jimbo la Darfur Magharibi Khamis Abubakar, alitoa wito wa uingiliaji wa kimataifa katika kile alichokiita mauaji ya kimbari.
Soma pia: Miili 180 yazikwa bila ya kutambuliwa kufuatia mapigano makali Sudan
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, alielezea wasiwasi wa katibu mkuu huyo juu ya kuongezeka kwa vurugu zenye mwelekeo wa ukabila pamoja na ripoti za vurugu za kingono.