1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miongoni mwa mambo ambayo Rais wa Nigeria Olusegun Obasanjo anataka kuhakikisha wakati akianza ziara yake ya Ujerumani Ijumaa ya leo, ni ni kuitoa nchi yake katika shutuma kwamba ni mojawapo ya nchi za mbele kabisa duniani katika balaa la rushwa

Ahmed M. Saleh8 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CHLw

Mjini Berlin Rais Obasanjo alilitembelea Shirika la Kupigana na Rushwa Duniani, TRANSPARENCY INTERNATIONAL. Kuhusu hali ya rushwa nchini Nigeria, gazeti la FRANKFURTER RUNDSCHAU linaandika: "Kipimo cha rushwa kinazidi kujitokeza barabarani ambako polisi huwakomoa watu pesa kwa sababu ya makosa madogo madogo tu. Hivi majuzi tu polisi walikamatwa mjini Lagos wakiwa na noti zilizokunjana mifukoni, wakati wakiwa kazini. Polisi hao hawakuchukuliwa hatua yoyote. Inadhihirika kuwa Wanigeria wengi wamekwisha yazoeya maisha ya rushwa. Lakini hasara kubwa kabisa ya kiuchumi inatiwa na rushwa iliyofichika, kuanzia sekta ya siasa hadi biashara ya mafuta. "Rushwa inasababisha asili miya ya matatizo yote ya Nigeria yanayolemaza uchumi wetu," aliandika Peter Obi, Mkurugenzi wa Zenith Bank Nigeria. Miaka mitatu iliyopita Rais Obasanjo akiunda Halmashauri ya Kupambana na Rushwa, ICPC. Tangu wakati huo hajahukumiwa afisa yeyote wa serikali au mwanasiasa kwa sababu ya ruhswa. Mbunge Mamman Ali siku moja aliingia bungeni na kumkabidhi Spika Dollar 20,000 na kumwambia, pesa hizo punde tu alipewa na watu asiowajua waliomwomba pesa hizo ni zake ikiwa atafuta mashtaka ya kuondolewa madarakani Rais Obasanjo, yaliyokuwa yaamuliwe bungeni kwa njia ya kura.
Visa vingi vya ulaji rushwa nchini Nigeria vimehusika na biashara za makampuni makubwa ya kimataifa, mwanachama wa Halmashauri ya Kupigana na Uhalifu wa Kiuchumi na Kifedha, aliliambia Shirika la IRIN. Kwa njia hiyo inasemekana kwamba tawi la Nigeria la kampuni ya Kimarekani HALLIBURTON hapo mwaka 2000 zililipa kiasi cha Dollar miliyoni 2,4 ili kiweze kupunguziwa mzigo wa kodi nchini Nigeria." Mabingwa wa UM wamegundua ishara halisi kuwa wanachama wa chama cha al-Qaida wanaendesha harakati zao kutokea Somalia. Gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG linaendelea kuandika: "Kwa mujibu wa ripoti ambayo wiki ijayo litakabidhiwa Baraza la Usalama la UM, lile shambulio la kujitolea mhanga lililofanywa mwaka uliopita katika Hotel Paradise mjini Mombasa, na lile jaribio la kuidengua ndege ya kiraiya ya Israel, ni njama zilizopangiliwa na kutekelezwa kutokea mji mkuu wa Somalia, Mogadishu. Wanachama wapatao wanne wa AL QAIDA wangaliko Somalia, wengine wakiweko Kenya. Pamoja na hayo ilisemekana kuwa silaha zimepenyezwa katika nchi hiyo kwenye Pembe ya Afrika kwa shabaha ya kupangiliwa mashambulio mengine. Japokuwa, muda tu baada ya shambulio la Septemba 11, Marekani iliitaja Somalia kama nchi watakamokimbilia magaidi wa AL QAIDA, lakini mpaka leo UM ukisisitiza kuwa nchi hiyo inatumiwa tu na magaaidi kupita njia. Lakini ripoti iliyochapishwa sasa ya UM inasisitiza kuwa kwa muda wa miaka kadha sasa chama hicho cha kigaidi kina vituo vyake nchini Somalia. Wafanya taftishi wamegundua kwamba hapo Agosti mwaka 2002, kikundi cha magaidi wa Al Qaida kilisafirisha kwa meli kutoka Somalia hadi Kenya, makombora mawili ya kushambulia ndege yaliyonunuliwa Yemen na makombora hayo kutumiwa Novemba 28 kwa shabaha ya kuidengua ndege ya abiria ya Kiisraeli. Makombora yote mawili yakishindwa kupiga shabaha yao. Lakini wakati huo huo waliuawa watu 15 katika shambulio lililofanywa HOTEL PARADISE. Magaidi wengi wanavutiwa na Somalia ambayo tangu mwaka 1991 haina utawala wake wenyewe. Pamoja na hayo nchini Somalia hufanywa biashara kubwa ya kuuza silaha zinazopenyezwa kutokea Yaman. Mabingwa wa UM wana hakika kuwa Fazul Abdullah Mohammed ndiye mkuu wa Al QAIDA nchini Smalia, akishutumiwa kupangilia njama za kushambulia Balozi za Marekani Saresalaam na Nairobi, 1998." Basi maoni hayo kutoka gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG; NI Ahmed Mohamed nikiwakamilshia makala hii ya AFRIKA KATIKA MAGAZETI YA KIJERUMANI.