Mionzi ya nyuklia yavuja Fukushima
26 Machi 2011Matangazo
Maafisa wa IAEA katika makao makuu, mjini Vienna wamesema kwamba mbali na vinu nambari 1 na 2, sasa data zinaonyesha kuwa hata katika mtambo nambari 3, kuna dalili za kuvuja kwa mionzi ya nyuklia.
Afisa mkuu wa IAEA anaehusika na masuala ya usalama wa nyuklia amesema, hatua kadhaa zinahitaji kuchukuliwa hata kabla ya kuanza kutathmini kiwango cha uharibifu uliotokea.
Hapo awali waziri mkuu wa Japan, Naoto Kan alisema kuwa bado kuna kazi kubwa sana ya kufanywa huko Fukushima .
Idadi ya watu waliopoteza maisha yao, kufuatia tetemeko kubwa la ardhi na tsunami nchini humo tangu majuma mawili yaliyopita, sasa imefikia 10,000 na watu wengine wapatao 17,000 bado hawajulikani walipo.